Wednesday, March 23, 2022

MWAKILEMA AWAVISHA VYEO MAKAMISHNA WAPYA TANAPA



KAMISHINA wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) William Mwakilema  amewavisha vyeo Makamishna Wasaidizi wa Uhifadhi waliopandishwa vyeo hivi karibuni katika tukio lililofanyika Hifadhi ya Taifa Ziwa Manyara.




Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Machi 23, 2022 na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Mawasiliano TANAPA Paschal Shelutete, waliovalishwa vyeo   ni pamoja na Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi Fidelis Kapalata na Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi Moses Nonga ambao kabla ya hapo walikuwa Maafisa Wakuu wa Uhifadhi.


Kamishna wa Uhifadhi William Mwakilema amewataka Makamishna wapya kufanya kazi zao kwa kuzingatia viapo vyao, weledi, bidii na maarifa ili kulifanya shirika lisonge mbele katika majukumu yake ya uhifadhi.



"Ni vema tufanye kazi kama timu moja kwa ushirikiano, tuwe mfano kwa tunaowaongoza pamoja na kuwajengea uwezo wa kushika nafasi za uongozi hapo baadaye," alisema  Mwakilema.

Kamishna Msaidizi Fidelis Kapalata kwa niaba ya mwenzake aliahidi ushirikiano kwa viongozi wenzake wa shirika ili kuweza kufikia malengo tarajiwa ya shirika.

No comments:

Post a Comment