Monday, March 14, 2022

MSHITAKIWA KESI YA SABAYA AELEZA NAMNA WALIVYOENDA KWENYE GEREJI YA MROSSO, ADAI SABAYA SI MTU MZURI


 


Mshitakiwa wa tatu, Watson Mwahomange,(27) kwenye kesi ya Ujuhumu Uchumi inayomkabili pamoja na Lengai Ole Sabaya ameieleza namna Sabaya alivyomfunga pingu na kwenda naye kwenye gereji ya Fransis Mrosso.

Aidha, ameomba mahakama itoe amri ya yeye kupatiwa ulinzi anaporudi gerezani kwa kile alichoeleza kuwa Sabaya ni mtu mbaya.

Watson anayejitetea mwenyewe baada ya wakili wake, Fridolin Bwemelo kujitete ameyasema hayo leo mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Patricia Kisinda anayesikiliza shauri hilo la uhujumu uchumi namba 27/2022 kwenye mahakama ya hakimu mkazi Arusha.

Ameeleza mahakamani hapo kuwa ni kweli Januari 20, 2021 alienda kwenye gereji ya Mrosso kwa ajili ya kutengeneza pampu kama alivyotumwa na Sabaya ambapo alikipa kiasi cha shilingi 100,000 lakini walishindwa kumps risiti  ya EFD kwani mashine yao ilikuwa mbovu baada ya kujaribu kutoa risiti hiyo mara kadhaa na kushindikana.

Watson alidai kuwa baada ya hapo alipiga picha risiti aliyopewa ikiwa na picha ya aliyemuhudumia kisha akamtumia Sabaya ili athibitishe kuwa alienda kwenye gereji hiyo na si za mtaani kama alivyokuwa akidai kisha akampa pampu hiyo mtu aliyemletea yeye akabaki Arusha.

Akadai kuwa siku mbili baadaye alipigiwa simu na mshitakiwa wa tano, Silvester Nyegu akimweleza afike hoteli ya Point Zone anaitwa na Sabaya ambapo yeye alichelewa kufika hali iliyosababisha akutane getini na msafara wa magari ya Sabaya uliokuwa na magari tatu ikiwemo moja la serikali na mengine mawili ikiwemo Prado na VX Masai.

Anadai Sabaya alichukizwa na hatua yake ya kuchelewa hivyo alimuagiza walinzi wake wawili amtoe lock kwa kumpiga makofi kwenye masikio yote kwa wakati mmoja kisha akamfunga pingu ilu asitoroke na kumweka kwenye ya magari aina ya VX Masai kisha msafara ukaelekea kwenye gereji ya Mrosso.

Watson anadai kuwa baada ya kufika yeye alibaki kwenye gari kwa muda kama nusu saa akiwa na pingu pamoja na dereva kisha akaitwa akaingia kwenye ofisi ya Mrosso ambapo alifunguliwa pingu aliporejea kwenye gari alikaa muda kidogo kisha dereva akaitwa ndani hivyo yeye akapata fursa ya kutoroka.

Anadai kuwa jijini Dar es Salaam alikamatwa akiwa na Sabaya, mke wake, mshitakiwa wa tano, Nyegu na mshitakiwa wa pili Enock Togolani wakiwa wamelala hotelini.

Watson alidai kuwa aliagizwa na Sabaya ampelekee begi lake lililokuwa na nyaraka jijini humo baada ya kumweleza kuwa yeyr anasafari ya kuelekea Dar hivyo baada ya kumkabidhi aliendelea kukaa kwenye hoteli aliyoshukia Sabaya ambaye alishauri kuwa muda umeenda sana hivyo akalale chumba wanacholala kina Nyengu na  Togolani ndipo usiku wakakamatwa.

SOMA ZAIDI...


Hakimu: Nataka unipe utetezi wako umesikia mashahidi wa  kwanza  hadi 13 na vielelezo unavikumbuka mahakama inataka katika utetezi wa tuhuma zinazokukabili kw kituo


Shahidi: Alikuja shahidi namba 10 ambaye ni Mfanyabiashara Francis Mrosso akaeleza tarehe, 20/1/2021nilikuwepo kwenye gereji yake iliyopo maeneo ya Mbauda hapa jijini arusha kwa ajili ya kutengeneza pampu. 

Mh hakimu nakumbuka siku hiyo 20.1.2021 nilikuwa nyumbani Sakina, majira ya asubuhi nikiwa bado nimelala nikapokea namba ngeni kwenye simu yangu baada ya kupokea ile namba ngeni ilikuwa sauti ya Sabaya ambaye ni mshitakiwa wa kwanza aliniambia dogo vipi?

Nikamjibu salama shikamoo mkuu,akaniuliza uko wapi nikamwambia niko nyumbani  akaniambia mwenye hii namba  anakuja Arusha kwa hiyo kuna mzigo wangu atakupatia amka ujiandae ukakutane naye.


Niliendelea kukaa nyumbani baada ya dakika 15 namba ile ilirudia kunipigia simu sauti ilikuja ya mtu mwingine.


Akaniambia kama nimepewa namba yako na mkuu wa wilaya ya Hai nakuja Arusha tukutane wapi?yeye anatokea Boma ng'ombe. Nikamwambia tukutane Florida. Nikamuuliza uko wapi akaniambia ndiyo anatoka Boma Ng'ombe.


Nikamwambia akikaribia Tengeru aniambie, akaniambia sawa baada ya dakika kama 45 yule bwana akanipigia nitoke yeye ndo amepita Tengeru



Nikajiandaa nikaita pikipiki akanipeleka Florida nikiwa kwenye pikipiki nilishuka nikatoa simy mfukoni ili nimpigie nikakuta missed call nne za huyo bwana.


Nikajaribu kumpigia simu yake ikawa inatumika,akamipigia akaniambia mbona unakua mswahili nimefika Florida nakupigia simu hupokei akaniambia njoo Mbauda.


Nikatoka na pikipiki hadi Mbauda nikampigia simu akaniambia niko na benzi nyeusi inawasha 'hazard' upande wa kushoto kabla ya kona ya Mbauda.


Baada ya kuangaza macho nikaona ile benzi nikamlipa dereva bodaboda nikaenda kwenye gari akashusha kioo akaniambia fungua mlango nikaingia kwenye gari.
Ilikuwa ndo mara ya kwanza kumuona huyo bwana.

Akaniambia kuna pampu nimepewa na Sabaya nikukabidhi ukasimamie itengenezwe akaniambai hii pampu inatakiwa itengenezwe shida yake haivuti nikamuuliza nikaitengenezee wapi akanielekeza yule bwana akageuza kichwa akaniambia nikivuka barabara kuna gereji nikamuuliza na.malipo ya hii pump inakuwaje nikashaambiwa malipo nitasema.


Nikabeba ile pump kwa boksi na nikasaidiwa na kijana nikaingia nae kwenye chumba ambacho kilikuwa kimegawanywa sehemu tatu


Nikafika nikakaa kwenye kiti nikamkuta mzee Shahidi namba nne,yule karani nilimkuta amevaa boshori ya bendera ya Tanzania na overoll la fundi 


Yule mzee akaiangalia ile pampu, nikamwambia ile pampu nimeagizwa nilete hapa tatizo lake haivuti kama nilivyokuwa  nimeelekezwa baada ya kumwambia akaniambia wataingiza kwenye mashine kupima ili tujue tatizo ni nini. Nikamwambia mzee sawa

Akachukua kitabu cha wateja akaniambia andika jina lako hapa,nikaandika Watson Stanฤบey pamoja na namba zangu za simu yule mzee akaipeleka pampy kwenye mashine.



Akawa amerudi baada ya dakika tano ikaletwa na shahidi namba 10.bwana Mrosso akawa ameorodhosha karatari ya vitu vilivyokufa na bei 45,000 kimoja,akawa ameandika grisi 5,000 na mashine yao kupima ni Sh 50,000.


Mrosso akawa ametoka nje nikabaki na yule mzee, Sabaya akawa amenipigia kwa aimu ya Sylvester akaniambia we dogo mimi nakutuma unaenda kuzunguka mtaani nakupigia simu hupokei nikamjibu mkuu nimepewa pampu nitengeneze nimeshakutana na huyo bwana akakata simu.


Kwa kuwa najua Sabaya ni mtata nikamuomba yule mzee naomba kupiga picha hii gharama nimtumie aliyeniagiza yule mzee akaniruhusu na yule mzee akawa anaonekana kwenye ile picha ili nimthibitishie siko mtaani anakosema yeye.




Baada ya kumtumia ile meseji kwa kuwa nilikua nimetoka 'home' mapema nikamuuliza ni wapi napata chai nje huku nasubiria majibu akaniambia nikitoka nje kuna 'car wash' mkono wa kulia nitapata chai nikahudumiwa pale nikawa nimechomeka simu inaingia chaji huku natumia


Basi nilivyokaa muda kidogo yule jamaa aliyeenda Makuyuni nikamwambia pampu inahitaji laki moja kutengenezwa,baada ya muda kidogo nikatumiwa halopesa 105,000 nikatoa nikarudi gereji



No comments:

Post a Comment