ASASI isiyo ya Kiserikali ya HakiElimu kwa kushirikiana na Wananchi wamekamilisha Mradi wa Maji kwenye Shule ya Msingi Idilo wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma ambapo umegharimu kiasi cha shilingi Milioni 26.
Mradio huo umezinduliwa Machi 21, 2022 na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mpwapwa William Madanya, akiambatana na Mkurugenzi Mtendaji wa HakiElimu, Dkt. John Kalage, Walimu, Wanafunzi vinara, Wananchi pamoja na watendaji wengine wa Wilaya hiyo.
Kabla ya Mradi huo kukamilika wanafunzi walilazimika kuyafuata Maji umbali mrefu huku baadhi ya wasichana wakishindwa kuhudhuria masomo wanapokuwa Kwenye siku za hedhi.
Mradi huo pia utawasaidia wananchi ambapo Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Madanya ameagiza wananchi kuchangia kiasi kidogo cha pesa kila wanapochota Ili pesa hizo zisaidie kwenye uendeshani wa mradi huo na mahitaji mengine ya Shule.
Ametaja miradi ambayo inatarajiwa kufanikishwa kuwa ni pamoja na kilimo Cha mbogamboga na matunda, Bustani za maua na miti, ufugaji nakadhalika.
Shule ya Idilo ni Moja ya Shule ya Msingi inayotazamwa na HakiElimu kama Shule ya kuonyesha kwa vitendo nini kinapaswa kufanywa Ili kuboresha Elimu.




No comments:
Post a Comment