Monday, December 27, 2021

MFANYABIASHARA WA MADINI ANAYEDAIWA KUUAWA NA MWANAE AZIKWA, FAMILIA YATOA NENO

 


FAMILIA ya mfanyabiashara wa madini ya Tanzanite, Ruth Mmassy, (40) anayedaiwa kuuawa na mtoto wake, Patric (24) imesema kuwa tamaa ya mali huenda ikawa ndiyo chanzo cha mauaji hayo.
 
Kaka wa marehemu, Hamis Mmassy ametoa madai hayo leo wakati wa mazishi ya Ruth yaliyofanyika  nyumbani kwa wazazi wake katika kijiji cha Mikungani, Wilayani Arumeru, Mkoani Arusha.


Amedai tamaa za mali ndizo zimesababisha mtoto huyo kumuua mama yake.


“Marehemu hakuwa anaumwa alikuwa mzima wa afya, ndiyohivyo kama ulivyosikia kuwa mtoto wake wa kumzaa amemuua mama yake,” amesema Mmassy kwa masikitiko.


Akiongoza ibada ya mazishi Mchungaji, Ernest Mola wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, (KKKT) Usharika wa Mikungani,  alisema wanasikitishwa na tukio hilo na kuongeza kuwa  marehemu alikuwa mtu wa kujitolea.

“Mara ya mwisho alichangia usharika Shilingi milioni moja na tukashukuru kwa namna alivyojitolea kwa Mungu,” amesema Mchungaji Mola


Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji cha Mikungani, mwalimu Issa Salum amesema Ruth alisoma shule ya msingi Mikungani na alimfundisha kipindi akiwa mwalimu.


Kwa upande wa Mwenyekiti wa madalali wa madini , Jeremia Simon alielezea historia ya marehemu Ruth kuwa alizaliwa mwaka 1980 kwenye kitongoji cha Kairo mji mdogo wa Mirerani.


Marehemu Ruth Maasy enzi za uhai wake


Simon alisema marehemu alipotea kwenye Mazingira ya kutatanisha Desemba 11 mwaka huu na mwili wake  kugundulika Desemba 24, mwaka huu kwenye chemba la majitaka  nyumbani kwake Njiro, Kontena jijini Arusha akiwa amekufa.

Patrick Mmassy anayetuhumiwa kwa mauaji ya mama yake



Kamanda wa Polisi Mkoa Arusha , (RPC), Justine Masejo amethitisha jeshi hilo linamshikilia mtoto wa marehemu Patrick Mmassy( 24) kwa uchunguzi zaidi kihusiana na wa tukio hilo lililoibua simanzi kwa wakazi wengi wa jiji la Arusha.



No comments:

Post a Comment