Tuesday, November 16, 2021

RUFAA YA SABAYA YAPANGIWA JAJI, ITATAJWA DESEMBA

 

RUFAA ya aliyekuwa Mkuu wa wilaya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili imepangiwa kusikilizwa kwenye Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, mbele ya jaji, Butamo Philip kuanzia desemba 13, mwaka huu.

 


Wakili, Edmund Ngemela anayemwakilisha mrufani wa pili, Silvester Nyegu aliwaeleza  waandishi wa habari leo Novemba 16,2021 kuwa siku hiyo shauri hilo litafika mahakamani hapo kwa ajili ya kutajwa.

 

Rufaa hiyo iliyosajiliwa namba 129/2021 inatokana na kesi ya jinai namba 105/2021 ambayo ilisikilizwa kwenye mahakama ya hakimu mkazi Arusha na hakimu mkazi Mwandamizi, Odira Amworo ambapo Oktoba 15, mwaka huu walihukumiwa kifungo cha miaka 90 jela kwenye makosa matatu waliyokutwa na hatia.

 

 

Kifungo hicho ni adhabu ya miaka 30 jela kwa kila kosa walilokutwa na hatia ambapo kila mmoja alikutwa na hatia kwenye makosa matatu tofauti ya unyang'anyi wa kutumia nguvu na unyang'anyi wa kutumia silaha.

 

 

Hata hivyo mahakama iliamua adhabu hizo ziende kwa pamoja hivyo  kila mmoja atatumia kifungo cha miaka 30 jela.

 

Hata hivyo wakili Ngemela alisema kuwa wanasababu za rufaa zaidi ya 10 ingawa hakutaka kuingia kwa undani juu ya kile lilichopo ndani ya rufaa hiyo.

  

HUKUMU ILIKATIWA RUFAA


Awali hukumu hiyo ilitolewa na Hakimu Mkazi Mwandamizi Odira Amworo,  Oktoba 15,2021 majira ya saa 11:47 jioni baada ya kuanza kusoma hukumu hiyo kuanzia majira ya saa 5:56 asubuhi.

 

 amepewa adhabu kali ya kifungo cha miaka 90 baada ya yeye na wenzak wawili kupatikana na hatia ya kufanya makosa mawili ya unyang’anyi wa makundi na kosa moja la unyang’anyio wa kutumia silaha.

 

“Kama alivyosema wakili wa serikali mwandamizi, Felix Kwetukia kwamba mshitakiwa wa kwanza Lengai Ole Sabaya alikuwa mkuu wa wilaya aliyeteuliwa na Rais kitendo alichofanya kinadhalilisha taasisi ya Rais,” amesema Hakimu huyo na kuongeza.

 

…Na hakuna ubishi kwamba wote ni vijana na wanahitajika kama walivyoeleza mawakili wao na kwa mujibu wa sheria hakuna ubishi kwamba mikono yangu imefungwa naweza kuwafunga miaka 100 lakini kurudi chini siruhusiwi kufunga chini ya 30...

 

…Mbali ya kwamba wakili wa serikali ameomba viboko wachapwe na walistahili wachapwe manake nao walikuwa wanawatoa wenzao wenge…

 

(Mahakama kicheko)

 

…Lakini mawakili wenzetu wameshindwa kuinyambulisha sheria ya zamani ya watoto walikuwa wanapigwa viboko lakini sheria mpya hawapigwi viboko wamepenyea hapo angalau. Basi mikono yangu imefungwa adhabu ya chini

miaka 30 na viboko…

 

…Kosa la kwanza kila mshitakiwa miaka 30 kila mmoja kosa la pili miaka 30 kila mmoja na kosa la tatu miaka 30 kwa kila mmoja, kwa viboko mawakili wameshinda sitatoa viboko na adhabu ziende pamoja.Mna haki ya rufaa iko wazi,”.

 

 

 

 

 

 

No comments:

Post a Comment