Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini Kenya (DCI), George Kinoti, mehukumiwa kifungo cha miezi minne jela kwa kukaidi agizo la mahakama ililomtaka kurudisha bunduki za mfanyabiashara,Jimi Wanjigi .
Kinoti ametakiwa kujisalimisha kwenye gereza la Kamiti ndani ya siku saba na iwapo atakaidi agizo hilo, Mkurugenzi wa Mashtaka nchi Kenya, (DPP) ameagizwa kutoa hati ya kumkamata.
Mwanzoni mwa mwezi Januari 2019 mwaka huu, Kinoti alipewa siku 30 na Mahakama Kuu nchini humo kuhakikisha anarudisha bunduki na risasi zote zilizochukuliwa kutoka kwa mfanyabiashara, Wanjigi lilitolewa kama ilivyoagizwa mwaka 2019.
Mnamo Januari 2019 hakimu Anthony Mrima alikuwa ameagiza DCI Kinoti, Inspekta Jenerali wa polisi na DPP warejeshe bunduki zote na silaha ambazo zilichukuliwa katika makazi ya Wanjigi mjini Malindi mwaka wa 2017.
Tarehe ya kukabidhi silaha hizo kwa Wanjigi ilikuwa Machi 25, 2021 lakini amri hiyo ilikaidiwa na maafisa hao.
Jaji Chacha Mwita mnamo Juni 2019 alisema korti ilikosea kuzuilia silaha ya Wanjigi ilhali alikuwa na leseni halali ya umiliki.
Silaha zinazohitajika kurejeshewa mfanyabiashara huyo ni bastola moja, Smith & Wesson moja , bastola aina ya Glock, bunduki moja ya kivita kati ya zingine.
No comments:
Post a Comment