TAMIDA WAMPONGEZA JPM UDHIBITI WA MADINI NCHINI

 


Mwenyekiti wa Taifa wa TAMIDA, Sam Mollel


CHAMA Cha Wanunuzi na Wauzaji wa Madini nchini, (TAMIDA), wamempongeza Rais, John Pombe Magufuli kwa kufanikiwa kukomesha wizi, ulanguzi na utoroshaji wa madini uliokuwa unafanywa na wafanyabiasharawa madini wasio waaminifu na wazalendo.

Mwenyekiti wa Taifa wa TAMIDA, Sammy Mollel ameyasema hayo wakati akitoa salamu za mwaka mpya 2021.

Amesema kuwa katika kipindi cha miaka mitano tokea Rais, Magufuli aingie madarakani amekuza mchango wa sekta ya madini kwenye pato la Taifa na anaamini mpaka kufikia 2025  sekta ya madini itachangia asilimia 10 ya  pato la Taifa.

" Katika sekta ya madini pekee usimamizi na udhibiti waumeimarishwa sana. Amejenga ukuta wa Mererani na kuanzisha masoko ya madini ya serikali kila mkoa wenye madini," amesema Mollel na kuongeza.

"Kwa lengo la kukomesha wizi, ulanguzi na utoroshaji wa madini uliokuwa unaofanywa na baadhi ya wachimbaji na wafanyabiashara wa madini wasio waaminifu na wazalendo,".

Mollel amesema kwenye awamu hii ya pili ya Rais Magufuli, anaamini serikali itaendelea na uboreshaji wa usimamizi na udhibiti wa rasilimali za nchi ikiwemo sekta ya madini.

"Hii itafanya mchango wa sekta ya madini katika pato la Taifa kukua na kufikia malengo ya serikali ya kufikia asilimia 10 ifikapo mwaka 2015," amesema mwenyekiti huyo wa TAMIDA na kuongeza,

Mchango wa sekta hii usaidia uchumi wa Taifa letu kupaa na kutoka kwenye uchumi wa kipato cha kati kwa mataifa yaliyo na uchumi mdogo na kulifikisha Taifa kwenye uchumi wa kati wa kiwango cha juu kwa mataifa yenye uchumi unaoimarika kutokana na vigezo vya Benki ya Dunia,".




 
x

0 Comments:

Post a Comment