Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amemuagiza Kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Ruvuma, Hamza Mwenda ahakikishe anawakamata viongozi wa AMCOS kwa tuhuma za kutoa fedha za wanachama na kuwapa madiwani ili wakawashawishi madiwani wenzao wakubali kubadilisha eneo la ujenzi wa ofisi za Halmashauri ya Wilaya mji wa Mbinga mkoani Ruvuma.
Aliyasema hayo jana Januari 4, 2021 wakati akizindua jengo la Ofisi ya Halmashauri hiyo.
Madiwani waliohusika katika mvutano huo ni wa kata za Mkumbi (Bruno Kapinga), kata ya Lukalasi (Bosco Ndimbo) na wa kata ya Linda (Haule), ambao wanadaiwa kuchukua fedha kutoka kwa watendaji wa AMCOS kwa ajili ya kwenda kushawishi madiwani wenzao wakubali kuhamishwa kwa eneo la ujenzi wa makao makuu ya halmashauri hiyo.
Pia, Waziri Mkuu alikagua nyumba 7 za Wakuu wa Idara za Halmashauri ya Mji wa Mbinga zilizojengwa na Serikali kwa gharama ya sh. Milioni 321.771.
Awali ,Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga, Grace Quintine alimweleza Waziro mkuu kuwa lengo la miradi hiyo ni kuboresha mazingira ya makazi ya watumishi wa halmashauri ikiwa ni pamoja na kupunguza kilipa posho za nyumba kwa kila mwezi




No comments:
Post a Comment