Rais mpya wa Marekani Joe Biden ameanza kutengua sera kadhaa muhimu za Donald Trump, saa chache baada ya kuapishwa.
Rais Biden tayari amesaini maagizo ya watendaji 15 yanayolenga kukabiliana na kusambaa kwa virusi vya corona.
Amri nyingine ni kubadilisha msimamo wa utawala wa Trump juu ya mabadiliko ya hali ya hewa na uhamiaji.
Biden ameanza kufanya kazi katika Ofisi ya Oval baada ya kuapishwa mapema Jumatano kama rais wa 46 wa Marekani.
Kuapishwa kwa Biden kulikua na utofauti na nyakati nyingine yoyote kutokana na vizuizi vya coronavirus, na wachache walikuwepo kushuhudia viapo na sherehe.Donald Trump - ambaye bado hajakubali rasmi urais kwa Biden alikataa kuhudhuria hafla badala yake alikua na sherehe zake binafsi katika makazi yake.
Biden ameapa kuwa Rais wa Wamarekani wote sambamba na kuwa Rais anayefuata sheria ya katika ya nchi huku akizitaka jamii za kimataifa kuitegemea Marekani mpya.
Watangulizi wake watatu waliudhuria shughuli ya kuapishwa kwake: Barack Obama - ambaye bwana Biden alikuwa makamu wake wa rais kwa miaka nane - Bill Clinton na George W Bush, pamoja na aliyekuwa makamu wa rais wa Trump, Mike Pence.
Kamala Harris ameapishwa kama makamu rais wa bwana Biden. Ni mwanamke wa kwanza - mweusi kupata wadhifa huo nchini Marekani.
Ulinzi ulikuwa umeimarishwa zaidi katika shughuli hiyo katika jengo la Capitol baada ya wafuasi wa Trump kuvamia Januari 6.
Bwana Biden na mke wake bi.Jill Biden, pamoja na Bi. Harris na mume wake Doug Emhoff, walitembea kutoka katika makutano ya Pennsylvania mpaka Ikulu ya Marekani, wakiwasalimia marafiki na wafuasi wao.
Katika sherehe za uapisho huo zilijumuisha maonesho ya muziki ; Lady Gaga - aliimba wimbo wa taifa - pamoja na Jennifer Lopez na Garth Brooks.
Amanda Gorman, ni mwanamuashairi mdogo zaidi alirani shairi lake katika shughuli hiyo.Katika tamasha la jioni katika mji wa kumbukumbu wa Lincoln ulitumbuizwa na Tom Hanks pamoja na Bruce Springsteen, John Legend, Jon Bon Jovi, Justin Timberlake, na Demi Lovato.
Habari kwa msaada wa mitandao



0 Comments:
Post a Comment