RAIS, John Pombe Magufuli amempongeza Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, kwa kukubali kuwa miongoni mwa viongozi wa serikali inayoongozwa na Dkt Hussein Ally Mwinyi huku akidai maamuzi yake yaliokoa ndoa ya watu.
Kauli hiyo ameitoa jana Januari 14, 2020, Mkoani Geita, mara baada ya kumaliza kufanya mazungumzo na viongozi hao wawili waliomtembelea nyumbani kwake Chato.
Rais Magufuli amesema kuwa maamuzi ya Maalim Seif yalikuwa ya kishujaa na yenye mwongozo wa Mungu na jambo alilodai kuwa mwanga wa maendeleo ya Zanzibar umeanza kuonekana.
“Zipo ndoa ambazo zilivunjika hasa kule Pemba, labda mwanamke aliipigia kura na mwanaume akapigia ACT, na siku Maalim Seif ameingia kwenye serikali ndoa zile zikaungana, hii maana yake maamuzi yake yameunganisha wana ndoa na yana baraka kwa Mungu”, Rais Magufuli.
“Maalim Seif nataka nikuhakikishie uko kwenye serikali ambayo utaitumikia kwa moyo wako mwema na usishangae siku nyingine nikakualika kwenda kufungua mradi wowote na bahati nzuri nimepigiwa kura nyingi tu Zanzibar na mimi napanga ziara ya kwenda Pemba na Unguja kuwashukuru” Rais Magufuli

No comments:
Post a Comment