ABIRIA KUTOKA TANZANIA WAPIGWA MARUFUKU KUINGIA UINGEREZA


 UINGEREZA yapiga marufuku abiria kutoka Tanzania na Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuingia nchini humo ikiwa ni sehemu ya hatua ya  kuzuia maambukizi ya aina mpya ya virusi vya corona.

"Abiria wote kutoka Tanzania na Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo hawataruhusiwa kuingia nchini Uingereza na katika mataifa ya Irish kuanzia saa kumi alfajiri," amesema waziri wa usafirishaji nchini Uingereza, Grant Shapps, 

Kuanzia tarehe 22 Januari, saa kumi alfajiri wasafiri wote kutoka au wamepita nchini Tanzania ndani ya siku 10 hawataruhusiwi kuingia Uingereza na mataifa ya Irish, na wale ambao wana haki ya makazi nchini Uingereza na wanatoka Tanzania watahitaji kujitenga nyumbani kwao watakapowasili.

Katika masharti mapya nchini Uingereza dhidi ya Corona, lazima watu wabaki nyumbani au kusafiri, pamoja na kusafiri kutoka nje ya nchi labda tu ukiwa umeruhusiwa kwa kibali maalum kufanya hivyo.

Tanzana na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo zimeongezwa kwenye orodha ya Uingereza ya nchi zilizopigiwa marufuku ya wasafiri wake kuingia nchini huo kama hatua yza kudhibiti maambukizo ya aina mpya ya kirusi cha Corona kilichogunduliwa nchini Afrika kusini.

Marufuku hiyo itaanza rasmi Jumamosi na itakuepo kwa muda wa wiki mbili , serikali ya Uingereza imesema.

"Uingereza ilipiga marufuku wasafiri kutoka mataifa ya Afrika Kusini siku 10 zilizopita , mataifa hayo ni pamoja ni pamoja na Namibia, Zimbabwe, Botswana, Eswatini, Zambia, Malawi, Lesotho, Msumbiji na Angola - visiwa vya ushelisheli na Mauritius," taarifa kutoka idara ya usafirishaji imesema. 

Aliogeza kusema kuwa "Israel itaondolewa katika orodha ya mataifa yaliyopigwa marufuki kuingia Uingereza na watu waliowasili Januari 09 kutoka Botswana, Israel , Mauritius au visiwa vya shelisheli watahitajika kujitenga wenyewe kwa muda."

Awali Uingereza ilipiga marufuku abiria kutoka Afrika Kusini Desemba 24,na kuruhusu wale walio na visa pamoja na haki ya makazi nchini Uingereza na kuhitajika kujitenga kwa muda wa siku 10. 

Uingereza ni miongoni mwa mataifa ambayo yanakabiliana na janga la virusi vya corona kwa kiwango kikubwa na uchumi wake ukiwa umeyumba kutokana na wimbi la kwanza la virusi mambukizi ya corona.

0 Comments:

Post a Comment