Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Godfrey Mngereza, amefariki dunia usiku huu wa Disemba 24, 2020.
Taarifa za awali zinaeleza amefariki akiwa jijini Dodoma, lakini chanzo cha kifo chake bado hakijawekwa wazi.
Taarifa ya kifo chake zimethibitishwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Dr. Abbasi .
“Ni kweli amefia Hospitali, hamna mwenye taarifa za ziada hadi sasa, mwenyewe nimeshtushwa” - Dr. Abbasi.


0 Comments:
Post a Comment