Mlima Kilimanjaro ni mlima mrefu kuliko yote barani Afrika na unapatikana wilaya ya Moshi, Rombo, Siha na Hai mkoani kilimanjaro.
Mkuu wa wilaya ya Moshi,AlhajiRajab Kundya akimkabidhi bendera Kanali, Martin Kibiriti ambaye aliongoza msafara wa watu 49 kuelekea kilele cha mlima Kilimanjaro kuanzia Desemba 5, mwaka huu .
Safari hiyo ya siku sita kuelekea kwenye kilele cha mlima Kilele cha mlima Kilimanjaro kupitia lango la Marangu kusimika bendera ya Tanzania ikiwa ni maadhimisho ya miaka 59 ya uhuru wa Tanganyika.
Msafara huo ulijumuisha wanajeshi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania, (JWTZ), Waandishi wa habari na wajumbe wa bodi ya Wadhamini, pamoja na wafanyakazi wa hifadhi za Taifa, (TANAPA).
Kauli mbiu ya mwaka huu MLIMA NI SALAMA PANDA UKIWA TANZANIA.
Kampuni ya ZARA ndiyo iliyotoa huduma kwenye msafara huo, muongozaji watalii wa kampuni hiyo, Chombo alisaidiwa na waongoza watalii wasaidizi na wapagazi kuhakikisha msafara huo unafika kileleni.
Nikiwa miongoni mwa waandishi waliopanda mlima huo, tulianza safari majira ya saa tano asubuhi. Tulielekezwa kuvaa mavazi mapesi na viatu vizivyobana miguu kama raba vitakavyokupa uhuru wa kutembea.
Mbele kabisa alikuwa Chombo ambaye alituelekeza kutembea kwa mstari mmoja ambapo mwendo tuliokuwa tukitembea ni taratibu na kwa kuwa muongozaji alikuwa mbele yeye ndo alikuwa anadhibiti hilo.
Wakati tumeanza safari hatua chache kutoka lango la Marangu tuliingia kushoto ambapo kila mmoja alikuwa na begi dogo la mgongoni lililobeba mahitaji muhimu kwa ajili ya mlima.
Huko tuliweka koti dogo la kuzuia mvua na koti refu la kuzuia mvua, maji, pamoja na chakula cha mchana tulichokabidhiwa.
Siku hiyo tulitembea kwenye ukanda wa misitu minene ya mlima huo tukiwa tunasikia sauti za maji yanayotiririka pamoja na milio ya ndege wa aina mbalimbali.
Majira ya saa tisa alasiri tulikuwa eneo la ??....... ambalo tulipumzika kwa ajili ya watu kula na kupata huduma za vyoo. Binafsi nilichukua fursa hiyo kumuona mtu wa huduma ya kwanza kutoka hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro ,
tuliyekuwa tumeongozana naye.
Nilipata maumivu ya msuli kwenye mguu wa kulia hivyo alinipaka dawa ya kuchua maumivu yakapungua tukarudi kwenye msafara kuendelea na safari.
Tulianza safari nilikuwa katikati lakini baada ya mapumziko nilijikuta niko nyuma kwani watu walipoanza kujipanga nilikuwa napatiwa huduma ya kwanza.
Nikurudishe nyuma kidogo kabla hatujafika eneo la kupumzika nilipoanza kubadili mwendo kuonesha nina maumivu ya mguu muongozaji watalii alinifuata na kuniomba anisaidie kubeba begi.
Muongoza watalii huyo ambaye baadaye aliniambia anaitwa Gibri mbali ya kubeba begi langu alikuwa na begi lingine kubwa amebeba mgongoni ambapo kwa haraka unaona mtungi wa hewa ya oksigeni.
Aliyembea pembeni yangu akitaka kujua shida inayonikabili. Nikamwambia mguu unauma akanishauri tupunguze mwendo ila nikaamua kukomaa na mwendo wa wenzangu kwani maumivu hayakuwa makali sana.
Alikuwa ananihimiza kunywa maji kidogo kila baada ya muda mfupi kweli niliona yalikuwa yakinipa nguvu ya kuendelea na safari mpaka tukafika eneo la kupumzika.
Tuendelee baada ya kula tuliendelea na safari ya kuelekea Mandara ambayo ni kilometa nane kuanzia geti la Marangu. Tulipokuwa tunatembea ni kama tambarare huwezi kujua kama unaoamba mlima ila kwenye maeneo machache ndiyo kulikuwa na miinuko ambayo ukiiangaliz unajua hapa tunapanda.
Tulifika Mandara saa 12 jioni tukapiga picha ya pamoja muongoza watalii kiongozi, Chombo akatupa maelekezo namna tutapata huduma ya chakula na malazi tukiwa Mandara kisha tukaelekea kwenye vyumba kama tulivyoelekezwa .
Tukiwa vyumbani tuliletewa maji ya uvuguvugu kwa ajili ya kufuta jasho tukabadili nguo tukaenda kupata mlo wa usiku ambao ulikuwa umeandaliwa vizuri.
Baada ya hapo tulienda kulala ambapo tulitakiwa kuwa tayati kwa ajili ya kupata chai saa mbili kamili siku inayofuata.


0 Comments:
Post a Comment