Monday, August 28, 2017

UPDATES: Sentensi tatu 3 za Mbunge Msukuma kuhusu Tundu Lissu kuwataka Mawakili Kugoma

”Watanzania kwa pamoja tunalaani kitendo kilichofanywa kwenye Ofisi za IMMMA Advocates kwa sababu ni kitendo cha kinyama na kihalifu. Tunamuomba IGP Sirro afanye juu chini kuhakikisha watu hawa wanakamatwa.
“Nilishtushwa sana na matamko yaliyotolewa na Rais wa TLS, Tundu Lissu jana kwamba anatangaza mgomo wa Wanasheria kuanzia kesho na keshokutwa. Najiuliza kama Tundu Lissu anatangaza mgomo wa Wanasheria, hiyo ndiyo hukumu ya kumpata mvamizi?
“Nadhani Wanasheria waisaidie Polisi kumgundua ni nani. Kama kuna taarifa Tundu Lissu mpaka anafikia kusema tukigoma atapatikana aliyefanya haya matendo, aisaidie Polisi waweze kumkamata haraka.” – Joseph Msukuma.

No comments:

Post a Comment