JAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI
YA RAIS
TAWALA
ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

Anwani
ya Simu “REGCOM”
OFISI YA MKUU WA MKOA,
Simu: 2545608/2545820/2545872
P.O. BOX 3050,
Fax: 2545239/2544386
21 /08/2017
ARUSHA.
TANGAZO LA MKOPO KWA WANAWAKE WA JIJI
LA ARUSHA
1.0 Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Arusha kupitia
fedha za marejesho ya pikipiki za UBOJA (Revolving funds) anawatangazia
wanawake wa Jiji la Arusha kuwa anatarajia kuwawezesha wanawake 500 ambao ni wafanyabiashara
wadogowadogo au wanaotegemea kuanza biashara ndogondogo kwa ajili ya kujikimu
kimaisha kwa kuwapatia kiasi cha Tsh
200,000/=kama mkopo usiokuwa na riba na masharti magumu. Mkopo huu utalenga
mwanamke mmoja moja/ kundi la wanawake watakao timiza vigezo.
2.0 VIGEZO VYA KUPATA MKOPO
I. Awe/Wawe wanawake wenye kipato cha
chini, kundi la wanawake waliopo kwenye Biashara ndogondogo.
II. Wawe wenye mawazo ya kufanya Biashara
na hawana mtaji wa kuanzisha biashara zao.
III. Kipaumbele cha mkopo huu ni kwa
wanawake wajane na yatima.
IV. Wawe wakazi wa Kata husika na Mtaa
husika ndani ya Jiji la Arusha, awe anafahamika/anatambulika kwa viongozi wake
wa mtaa yaani Mtendaji wa mtaa.
V. Asiwe na mkopo kutoka mahali pengine
ili kurahisisha marejesho yake ya kila wiki.
VI. Awe na wadhamini wawili (2)
wanaofahamika ndani ya Mtaa na Kata husika
3.0 Wanawake wote watakao kidhi vigezo tajwa
hapo juu mnakaribishwa kuwasilisha maombi yenu ya mkopo katika Ofisi ya Kata
unayoishi, maombi hayo yaambatanishwe na
utambulisho wa Mtendaji wa mtaa
unaoishi.
4.0
Mwisho wa kuwasilisha maombi ni siku kumi na nne(14) kuanzia tarehe ya
tangazo hili tarehe 21/o8/2017 hadi tarehe 4/9/2017, na bahasha za maombi
zitafunguliwa mbele ya waombaji watakao penda kuhudhuria.
5.0 Taarifa za matokeo ya waliofanikiwa
kupata mkopo zitatolewa kupitia Ofisi za Kata baada ya uchambuzi wa kina
kufanyika kwa kuzingatia vigezo vilivyo ainishwa.
6.0
wanawake watakao fanikiwa
kukidhi vigezo vya mkopo watapewa mafunzo ya ujasiriamali bure kabla ya kupewa
mkopo.
7.0 NAMNA YA KUREJESHA MKOPO
I. Marejesho yatafanyika kwa kipindi cha miezi mine (4) ukiwepo mwezi
mmoja (1) wa Matazamio hivyo muda wa
kukamilisha marejesho utakuwa ni kipindi cha miezi mitano (5)
II. Fedha zote za marejesho zitapelekwa Benki kwenye akaunti
maalumu itakayofunguliwa kwa ajili ya marejesho ya mikopo hiyo.
Mnakaribishwa kwa maombi.
Imetolewa na
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
No comments:
Post a Comment