Haberturk : « Tahadhari kwa Marekani kuhusu FETÖ na PYD »
Rais wa Uturuki amemtahadharisha waziri wa ulijnzi wa Marekani James Mattis katika ziara yake rsmi nchini Uturuki kuhusu serikali ya Marekani kutoa msaada kwa kundi la wanamhgambo wa PYD. Uturuki inathumu kundi hilo kuwa tawi la kundi la kigaidi la PKK. Marekani inatoa msaada wa kijeshi kwa wanamgambo hao kwa kudai kuwa kudni hilo ni mshirika katika kupambana na makundi ya kigaidi nchini Syria na Iraq. Kundi la PYD limepewa silaha na Marekani kwa ajili ya kupambana na kundi la Daesh. Uturuki imezungumzia kuhusu kundi la FETÖ na kiongozi wake kurejeshwa nchini Uturuki kutokana na kuhusika kwake katika jaribio la mapinduzi la Julai 15 mwaka 2015. Rais Erdoğan amesema kuwa kura ya maoni katika eneo la wakuridi nchini Iran katika maeneo yanayomilikiwa na PYD ni jambo lisilokubalika.
Vatan : « Uturuki na Viet Nam ni mataifa yanayoshirikiana bega kwa bega »
Waziri mkuu wa Uturuki Binali Yıldırım afahamisha kwamba Uturuki itaendelea kufanya juhudi za kuboresha uhusiano wake na Vietnam. Yıldırım aliyafahamisha haya katika hafla ya mlo wa jioni iliyoandaliwa kwa ajili yake na Vietnam. Waziri huyo mkuu aliendelea kufahamisha kwamba katika siku za hivi karibuni Uturuki imekuwa ikifuatilia matukio ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini Vietnam. Aidha Yıldırım alikumbushia kwamba mwaka ujao watakuwa wanaadhimisha miaka 40 ya uhusiano wa kidiplomasia baina ya nchi hizo mbili. Waziri mkuu huyo pia alipendekeza kwamba mwaka 2018 uwe mwaka wa kitamaduni .
Yeni Safak : « Kituo cha utafiti wa anga»
Kitengo cha habari kuhusu safari za anga chaGokmen ambacho ni kittuo cha 5 ulimwenguni mjini Bursa kimehudhuriwa na naibu waziri mkuu Fikri İşik. Hatua ya kwanza ya mafunzo katika kituo hicho wanafunzi watakuwa na fursa ya kujifunza kuhusu anga na safari za mbali.
Hurriyet : « Yasemin Adar apajinyakulia medali ya dhahabu Paris»
Bingwa wa Mieleka Yasemin Adar ,mwanamke kutoka Uturuki amejishindia medali ya dhahabu katika michuano ya kimataifa inayoendelea Paris nchini Ufaransa . Yasemin Adar amekuwa mwanamke wa kwanza kushinda medali ya dhahabu katika mashindano hayo ya kimataifa baada ya kumshinda mwenzake kutoka Belarus kwa jina la Vasilisa Marzaliuk kwa 5 - 4 katika michuano ya wanawake katika uzani wa kilo 75. Baada ya kupokea medali yake ya dhahabu Adar alikubali pendekezo la ndoa kutoka kwa mpenzi wake Erdem YiÄŸit.
No comments:
Post a Comment