Kimbunga cha Noru chaelekea kisiwa kikuu cha Japani

Kimbunga cha Noru chaelekea kisiwa kikuu cha JapaniKimbunga kikali kiitwacho Noru kinaelekea katikati ya Japani baada ya kupita visiwa vya kusini magharibi mwishoni mwa wiki. Watu wawili wamefariki na wengine 16 wamejeruhiwa na kimbunga hicho.

Mpaka ilipofika saa tano asubuhi ya leo Jumatatu kimbunga cha Noru kilikuwa kimekaribia Rasi ya Muroto mkoani Kochi ulio kwenye la eneo la Shikoku. Kimbunga hicho kilikuwa kinaelekea kaskazini mashariki kwa kasi ya kilomita 20 kwa saa. 

Takribani watu 20,000 wameshauriwa kuondoka eneo hilo la Shikoku. Mamlaka zinawasihi wakazi wa maeneo hayo kujihadhari dhidi ya maporomoko ya udongo, mafuriko na kuongezeka kwa ukubwa wa mawimbi kwenye maeneo ya pwani.

Zaidi ya safari 220 za ndege zimeahirishwa na makampuni ya ndege yanasema idadi hiyo inaweza kuongezeka.

0 Comments:

Post a Comment