FULL VIDEO: Historia Tanzania na Marekani 'Miracles Childrens' Doreen,Saidia, na Wilson

Doreen Mshana
Kushoto) Wilson Tarimo, na Sadia Awadhi

Watoto walionusurika katika ajali ya Lucky Vincent Sadia Awadhi, Doreen Mshana  na Wilson Tarimo
 Leo wamepokelewa wakitokea nchini Marekani watoto hao ambao walikuwa wakisaidiwa na shirika la Samaritan purse la nchini Marekani wamerejea nchini wakiwa na afya imara tofauti na wakati walipokuwa wakienda kutibiwa ambapo halo zao zilikuwa mbaya.

Akizungumza wakati wa mapokezi ya watoto hao yaliyofanyika Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mama Anna Mghwira amesema serikali imekuwa bega kwa bega na wadau wote waliohusika katika kurejesha hali ya afya ya watoto hao. Akiwataja wadau hao ambao pia serikali imewakabidhi hati Maalum za kuwapongeza Madaktari wa shirika la Samaritan purse , na Mbunge wa Singida Kaskazini Mh. Lazaro Nyalandu.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Bi. Anna Mghwira akimkabidhi hati ya pongezi Mbunge Lazaro Nyalandu wa Singida Kaskazini ikiwa sehemu ya serikali ya kutambua juhudi zake nakimpongeza.

Katika mapokezi ya Saidia, Doreen  na Wilson ambao wametajwa kama watoto wa miujiza yaani 'Children of Miracles' viongozi mbalimbali waliweza kushiriki ikiwa ni pamoja na viongozi wa kisiasa wa hapa nchini na Taifa la Marekani ambapo kwa hapa nyumbani walishiriki viongozi wa vyama vya siasa , Wabunge akiwemo Joshua Nasari (MB) wa Arumeru Mashariki , Baadhi ya Madiwani kutoka Halmashauri ya jiji la Arusha wakiongozwa na Meya wa jiji hilo Mh. Kalisti Lazaro.  Huku kwa upande wa Taifa la Marekani alifika kwa niaba ya bunge la Congress la nchi hiyo katika tukio hilo la kitaifa.

VIDEO NZIMA IPO HAPA PLAY UONE- VOA TV NEWS

Tukio la Ajali ya Shule ya Lucky Vincent imekuwa ikichukua headlines kwenye vichwa vya Habari kote ulimwenguni.

Ndege ya Samaritan Purse imefika majira ya saa nne asubuhi katika uwanja wa kimataifa wa KIA,
Nakulakiwa na idadi kubwa ya watu wakiwemo wanafunzi wa shule ya Lucky Vincent , Wazazi wenza wa watoto waliopelekwa Marekani kwa matibabu. Pamoja na wadau mbalimbali walioguswa na Tukio hilo.

Endelea kusoma makala na matukio mbalimbali kote nchini hapa Habari Tanzania. Usisahau kutazama video zote za matukio ya hivi punde VOA TV - YouTube.

0 Comments:

Post a Comment