Tuesday, August 29, 2017

HABARI: CDA na ujenzi wa Dodoma

Serikali imesema itashughulikia utaratibu kwa watu waliouziwa viwanja na wale wanaotarajia kufanya kuuziwa viwanja hivi karibuni Mkoani Dodoma.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma Edwin Kunambi amebainisha hayo mbele ya Vyombo vya Habari mjini Dodoma.

“Manispaa ya Dodoma ilikabidhiwa jukumu la kuuendeleza Mji Mkuu wa Nchi. Shughuli zote ambazo zilikuwa zinafanya na iliyokuwa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu lakini zimekabidhiwa Manispaa ya Dodoma.
“Ni kweli kuna sintofahamu kwa Wananchi kwamba nini kinaendelea. Nitatoa habari kuwafahamisha Wananchi wa Manispaa ya Dodoma na Watanzania kwamba Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma tumeshachukua shughuli zote za CDA na tunaendelea kuzitekeleza kama kawaida.” – Edwin Kunambi.

No comments:

Post a Comment