
Baraza la Wanaake la Chama cha Demokrasia na Maendeleo BAWACHA Imezindua Jubilee iliyopewa jina la 'Silver Jubilee' akizungumza na VOA TV Leo Katibu wa Baraza hilo Arusha Bi. Irene Kimati amesema chama hicho kimefanikiwa kwa kiango kikubwa ambapo amesema hadi kufikia sasa kina idadi kubwa kuanzia Wabunge 4 na madiwani 42 mwaka 1995, Wabunge 5 na Madiwani 75 mwaka 2000 , Wabunge 11 na madiwani 103 Mwaka 2005, Wabunge 50 na Madiwani 467 mwaka 2010, Wabunge 72 na Madiwani 1108 Mwaka 2015 na Halmashauri 25 , Majiji Dar , Arusha , Mbeya na Iringa , Manispaa ya Moshi, na Mwanza.
Bi Irine ameeleza kuwa Pia katika kipindi cha maadhimisho ya miaka 25 ya Chama hicho pia chama hicho kimefanikiwa katika kipengele cha jinsia kwa maana ya Wanawake Wamepata fursa za kuiwakilisha jamii ipasavyo kuanzia kwenye majukwaa ya siasa na hadi bungeni .
Amesema katika maadhimisho ya miaka 25 ya CHADEMA Wanajivunia Wanaake kupewa fursa ipasavyo.
PLAY HII YA VOA TV VIDEO HAPA CHINI UJUE KILA KITU
No comments:
Post a Comment