Jeshi la Polisi wamemaliza upekuzi waliokuwa wanafanya nyumbani kwa Mwanasheria Mkuu wa Chama cha demokrasia na maendeleo Chadema Tundu Lissu na sasa muda anarejeshwa tena Kituo Kikuu cha Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa ajili ya taratibu zingine za kisheria kuendelea, ikiwa ni pamoja na dhamana yake ambayo kisheria iko wazi.
Upekuzi uliofanyika ulihusu makosa mawili anayotuhumiwa nayo ambayo ni;
1. Kusema makosa ya rais hadharani.
2. Uchochezi kuhusu kushikiliwa ndege ya Tanzania aina ya Bombardier Q400 huko nchini Canada.

0 Comments:
Post a Comment