Ripoti za kuaminika zinasema kuwa, mrithi wa kiti cha ufalme wa Saudi Arabia na mwana wa mfalme wa nchi hiyo, Muhammad bin Salman amekoswakoswa kuuawa kwa risasi ndani ya familia ya kifalme ya Saudia.
Hayo yamethibitishwa na mtaalamu wa masuala ya kisiasa na ya kimataifa Dakta Hazam Hazam ambaye amefichua kwamba, Muhammad bin Salman amefyatuliwa risasi na watu wa ndani ya falimia ya kifalme ya Saudi Arabia.
Dakta Hazam ambaye yeye mwenyewe ni raia wa Saudi Arabia amesema kuwa, sababu ya kutoonekana hadharani mrithi huyo mpya wa kiti cha ufalme tangu baada ya kuchaguliwa na baba yake baada ya kumbwaga na kumuuzulu Muhammad bin Nayif, ni hali tete na isiyokuwa na utulivu inayotawala familia ya kifalme ya Saudia.
Dakta Hazam amongeza kuwa, mivutano na hitilafu baina ya mirengo na makundi hasimu ndani ya familia ya kifalme ya Saudi Arabia imepamba moto baada ya kuchaguliwa Muhammad bin Salman kuwa mrithi wa kiti cha mfalme na yaliyojiri baada yake na ripoti zinasema mmoja kati ya watoto wa Muqrin bin Abdul Aziz alifyatulia risasi Muhammad bin Salman na mmoja kati ya ndugu zake ambaye amejeruhiwa vibaya. Ripoti zinasema Muhammad bin Salman mwenyewe amepigwa risasi mkononi.
Mtaalamu huyo wa masuala ya kimataifa anasema, picha zinazoonyeshwa kwa sasa za Muhammad bin Salman si za sasa. Amesema kuwa vikao vimekuwa vikifanyika kila siku ndani ya ukoo unaotawala wa Aal Saud ili kupata suluhisho la hitilafu na mivutano hiyo na kwamba juhudi hizo bado hazijazaa matunda. READ MORE
No comments:
Post a Comment