Baada ya kuwepo kwa taarifa ya kutoonekana kwa Maneja wa kitengo cha ICT ya Tume ya uchaguzi na mipaka ya Kenya IEBC , Chris Musando ... Taarifa mpya leo ni kwamba Mwili wa Maneja huyo umepatikana ikiwa amefariki.
Imeelezwa kuwa mwili wa Chris Musandoaliyekuwa Meneja wa masuala ya Teknolojia wa IEBC, umehifadhiwa kwenye chumba cha kuhifadhi maiti mjini Nairobi huku mawasiliano yake ya mwisho yakiwa kwa njia ya SMS na mmoja wa wafanyakazi mwenzake siku ya Jumamosi majira ya saa tisa usiku.
Tukio hili linatokea ikiwa imesalia wiki moja kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu Kenya ambao utafanyika tarehe 8 August.
Polisi wanasema kuwa miili ya Afisa huyo pamoja na mwanamke ambaye hakutambuliwa, ilipatikana eneo la Kikuyu lililo vitongoji vya mji wa Nairobi na kupelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti.

No comments:
Post a Comment