Tuesday, July 11, 2017

UGAIDI: Uturuki imesema imewaua magaidi 11 wa PKK


Jeshi la Uturuki limeeleza kuwa limefanikiwa kuwaangamiza magaidi 11 wa PKK huko kusini mashariki mwa Uturuki.
Kwa mujibu wa taarifa, zinaeleza kuwa kati ya hao, magaidi 8 waliuawa katika jimbo la Mardin ambapo inasadikika kuwa walikua tayari kuandaa shambulizi. Wengine watatu waliuawa katika jimbo la Hakkari.
Kundi la PKK ambalo  Marekani, Uturuki pamoja na Umoja wa Ulaya unalitambua kama kundi la kigaidi lilanzisha upya kampeni zake za kigaidi dhidi ya Uturuki mwezi Julai mwaka 2015.
Tangu mwaka 2015, PKK imehusishwa na mauaji ya takriban watu 1200  ikiwa ni pamoja na wanajeshi, wananchi wa kawaida wakiwemo wanawake na watoto.

No comments:

Post a Comment