Wito wa Rais Erdogan wa Uturuki kwa Uislamu ulimwenguni

Rais Recep Tayyıp Erdoğan ametoa wito kwa waislamu wote ulimwenguni kuchukua hatua ili kulinda hadhi ya msikiti mtukufu wa Al Aqsa .
Hasira imezuka Ukingo wa Magharibi tangu juma lililopita baada ya Israel kufunga msikiti wa Al Aqsa na kuzuia waislamu Jerusalem kutofanya ibada zao katika msikiti huo.
Msikiti huo ulifunguliwa tena baada ya siku mbili kisha vyuma vyenye vifaa vya kuhisi silaha hatari na kamera za ufuatiliaji kuwekwa katika lango kuu la msikiti huo.
Rais ErdoÄŸan alitoa wito huo Juanne alipokuwa anahutubia wanachama wa chama tawala cha AKP mjini Ankara .
ErdoÄŸan aliendelea kusema kwaamba hatua ya kulinda Al Aqsa sio jukumu la kawaida tu bali pia ni jukumu la kiimani .
Alitoa wito kwa waislamu walio na uwezo wa kuzuru Al Aqsa wafanye hivyo na wale wasio na uwezo wapeleke misaada kwa ndugu zao wa kiislamu katika kanda hiyo

0 Comments:

Post a Comment