Mahakama ya Hakimu Mkazi KISUTU imetupilia mbali ombi la kumnyima dhamana mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu hivyo kutoa fursa kwa mbunge huyo kudhaminiwa
Uamuzi huo umetolewa leo asubuhi na hakimu Mkazi Mkuu Wilbard Mashauri baada ya kujiridhisha kuwa upande wa mashtaka umeshindwa kutaja kesi ambayo Lissu aliwahi kuruka dhamana.
Alisema kuwa hoja ya kutaka Lissu anyimwe dhamana kwa ajili ya usalama wake haijitoshelezi kumuweka ndani.
Alisema Lissu kitendo cha kundi la Mawakili 18 kujitokeza kumuwakilisha inaonesha watu wanaupendo dhidi yake.
Lissu amepewa masharti ya dhamana yanayomtaka kuwa na wadhamini wawili wanaoaminika ambao watasaini bondi ya sh 10 milioni kila mmoja.
Pia ametakiwa asitoke nje ya jiji Dar es Salaam bila ya kuwa na kibali cha mahakama.
Kesi ililazimika kuahirishwa kwa muda kusubiri wadhamini ambao walifika lakini kutokana na ulinzi ulioimarishwa mahakani hapo na askari polisi walizuiwa kuingia ndani ya Mahakama

No comments:
Post a Comment