"Press release"
Kamati Kuu ya CHADEMA imekutana kwa siku mbili, tarehe 29-30 Julai, 2017 katika Hotel ya Double Tree, jijini Dar es Salaam.
Kikao hicho kimejadili na kufikia maazimio na hatua za kuchukua katika ajenda zifuatazo;
1. Hali ya mwenendo wa siasa katika nchi na ukandamizaji wa demokrasia unaofanywa na serikali ya awamu ya tano.
2. Kuporomoka kwa uchumi na hali ngumu ya maisha kwa Watanzania
3. Kamata kamata inayoendelea kufanywa na vyombo vya dola dhidi ya viongozi, wanachama na wafuasi wa CHADEMA maeneo mbalimbali nchi nzima.
Taarifa kamili juu ya maazimio hayo na hatua zitakazochukuliwa na Chama itatolewa kesho Jumatatu tarehe 31 Julai 2017, kwenye kikao na waandishi wa habari kitakachofanyika jijini Dar es salaam.
Imetolewa na John Mrema
Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje.

0 Comments:
Post a Comment