Lengo la muswada huu kufanyia marekebisho sheria mbalimbali za kikodi na nyinginezo ili kuwezesha utekelezaji wa kisheria wa Bajeti ya Serikali wa mwaka 2017/18-Mhe. Dkt. Mpango
Muswada huu unakusudia kuzifanyia marekebisho Sheria kumi na tano-Mhe. Dkt. Mpango
Muswada huu unakusudia kupunguza kiwango cha ushuru wa bidhaa kwa baadhi ya bidhaa zinazozalishwa nchini.-Mhe. Dkt. Mpango
Muswada huu utaweka utaratibu wa kudhibiti utoaji wa madini migodini kwa ajili ya usafirishaji nje ya nchi au kwa matumizi ndani ya nchi-Mhe. Dkt. Mpango
Kupanua wigo kwa kutoa fursa kampuni,watanzania wanaoishi nje ya nchi,taasisi za nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki kununua hisa za kampuni za mawasiliano-Mhe. Dkt. Mpango
Kuweka utaratibu wa kuwatambua rasmi,washereheshaji kwenye sherehe, watoa huduma ya chakula, wafanya biashara wadogo wasio rasmi kwa kuwapatia vitambulisho maalum vya kazi-Mhe. Dkt. Mpango
Muswada huu kwa kiwangi kikubwa umezingatia mawazo na mapendekezo ya wadau mbalimbali wakiwemo wabunge,wafanyabiashara, wamiliki wa viwanda, na taasisi binafsi na za Serikali-Mhe. Dkt. Mpango
Muswada huu utapunguza kiwango cha ushuru kwa bidhaa zinazozalishwa nchini-Mhe. Dkt.Mpango
Kutoa msamaha wa kodi ya ongezeko la thamani kwa magari yanayotumika kwa ajili ya kubeba wagonjwa-Mhe. Dkt. Mpango
Muswada huu utapunguza ushuru wa mazao unaotozwa na halmshauri za Wilaya kutoka kiwango cha asilimia 5 ya thamani ya mauzo hadi asilimia 3 kwa mazao ya biashara-Mhe. Dkt. Mpango
Muswada wa sheria ya fedha wa mwaka 2017 (The Finance Act 2017) umepitishwa na Bunge jioni hii.
IMEANDALIWA NA IDARA YA HABARI- (MAELEZO)
No comments:
Post a Comment