Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini amekanusha madai ya kumiliki kasri katika Umoja wa Falme za Kiarabu au Imarati.
Katika taarifa iliyotolewa kupitia ofisi yake, Zuma amekanusha ripoti za vyombo vya habari kuwa familia moja tajiri imemnunulia kasri hiyo huko Imarati.
Zuma anazidi kushinikizwa ajiuzulu kutokana na tuhuma za kuhusika na ufisadi huku nyaraka laki moja zilizovuja wiki jana zikidai rais huyo amehusika na ufisadi. Hivi karibuni Zuma alinusurika katika kura ya kutokuwa na imani naye katika kamati kuu ya chama chake tawala cha ANC. content ya ParsToday
Gazeti la Sunday Times la Afrika Kusini limedai kuwa familia ya Gupta imemnunulia Zuma nyumba ya kifakhari mjini Dubai inayokadiriwa kugharimu dola milioni 25.
Gupta mwenye asili ya India ni tajiri mkubwa Afrika Kusini na amehusishwa na kashfa kadhaa za ufisadi ambazo amezikanusha na kusema kuwa habari zinazoenezwa dhidi yake ni 'bandia.'
0 Comments:
Post a Comment