Mahakama ya pili ya serikali kuu ya Marekani imetoa uamuzi wa kuendelea kupinga amri ya kiutendaji iliotolewa na Rais Donald Trump ya kuzuia wahamiaji kutoka mataifa 6 ya Kiislamu kuingia hapa Marekani.
Majaji kwenye Mahakama ya 9 ya rufaa iliyoko San Francisco wamekubaliana kwa pamoja jumatatu dhidi ya amri ya Trump wakisema kuwa Rais alitumia mamlaka kupita kiasi wakati alipochukua hatua hiyo Machi 2.
Jopo la majaji watatu limesema kuwa ingawa sheria ya uhamiaji ya 1952 inampatia rais uwezo mkubwa wa kudhibiti watu wanaoingia marekani pamoja na kulinda raiya wa marekani, hatua za uhamiaji hazichukuliwi na mtu mmoja kama alivyofanya.
Uamuzi wa jumatatu umefuatia ule wa mahakama ya rufaa ya Virginia mei 25 ambao ulikubaliana na uamuzi wa awali uliofanywa na jaji wa Maryland ukizuia sehemu za amri ya Rais.
Hata hivyo mahakama hizo zimetoa hoja tofauti wakati wa kufanya maamuzi hayo.
No comments:
Post a Comment