UPDATES: Obama aukosoa uamuzi Wa Trump kujiondoa Makubaliano ya


Aliyekuwa Raisi wa Marekani Barack Obama amekosoa uamuzi wa mrithi wake Donald Trump, wa kuondoa Marekani kutoka kwa makubaliano ya Paris juu ya mabadiliko ya tabia nchi.

Katika taarifa yake jana Alhamisi, amesema kwamba makubaliano hayo yaliwezeshwa kufikiwa na uongozi thabiti na wenye maadili mema wa Marekani.

Obama amesisitiza kwamba uvumbuzi binafsi wa Marekani na uwekezaji wa umma katika viwanda vinavyoendelea kukua kama vile vya upepo na nishati ya jua viliunda baadhi ya mikondo mipya ya ajira zenye malipo mazuri katika miaka ya hivi karibuni na kuchangia uzalishaji ajira za muda mrefu katika historia ya Marekani. 

Amesema kwamba sekta za kibinafsi tayari zimechagua hatma ya baadaye yenye kiwango kidogo cha hewa chafuzi kwa mazingira.

Ameongeza kuwa hata wakati ambapo utawala wa sasa nchini humo unapoungana na nchi chache ambazo zinapinga hatma hiyo, ana imani kwamba Marekani na sekta ya kibiashara zitaweka juhudi zaidi kuwa katika mstari wa mbele na kusaidia kulinda sayari ya dunia kwa kizazi kijacho.

0 Comments:

Post a Comment