Wednesday, June 7, 2017

UPDATES: Mfalme wa Kuwait awasili Saudia Sakata la Qatar

Kiongozi wa Kuwait anazuru nchini Saudi Arabia akijaribu kutatua mpasuko wa kidiplomasia kati ya Qatar na mataifa ya Kiarabu.

Mfalme wa Kuwait, Sheikh Sabah Al Ahmed Al Sabah, aliwasili mjini Jeddah jana Jumanne ambapo atakutana na Mfalme Salman bin Abdulaziz wa Saudi Arabia.

Nchi kadhaa zikiwemo Saudi Arabia na Milki za Kiarabu-UAE, zimesitisha uhusiano wa kidiplomasia na Qatar zikiihusisha nchi hiyo na makundi yanayoungwa mkono na Iran.

Taarifa za vyombo vya habari zinasema kuwa benki za nchini Saudi Arabia na UAE zimesitisha mihamala ya kifedha na Qatar na serikali ya Saudi Arabia inayataka makampuni yake kujiondoa nchini humo.

Kuwait, Saudi Arabia, Qatar na UAE ni miongoni mwa nchi wanachama wa mataifa sita yanayounda Baraza la Ushirikiano wa mataifa ya Ghuba.

No comments:

Post a Comment