Naibu wa Kamanda wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran (SEPAH) amesema kuwa, Iran italipiza kisasi cha damu ya mashahidi waliouawa katika mashambulio ya kigaidi ya jana mjini Tehran.
Brigedia Jenerali Hussein Salami amesebainisha kwamba, Iran haitakaa kimya bali italipiza kisasi cha damu ya mashahidi hao kwa magaidi, watu wanaofungamana nao na waungaji mkono wao.
Naibu wa Kamanda wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran (SEPAH) amewaambia waandishi wa habari kwamba, magaidi wanapaswa kufahamu kwamba, Iran haitasimamisha hata kidogo vita vyake dhidi ya magaidi. Brigedia Salami amezungumzia mashambulio ya jana ya kigaidi katika jengo la ofisi za Bunge na katika Haram ya Imam Khomeini (MA) na kusifu operesheni ya vikosi vya usalama iliyohitimisha tukio la shambulio la kigaidi katika jengo la ofisi za Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran).
No comments:
Post a Comment