Mwanzoni mwa mkutano huo Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Utokomezaji Silaha za Nyuklia, Izumi Nakamitsu, amesema utokomezaji wa silaha za nyuklia umekuwa ni lengo la muda mrefu la Umoja wa Mataifa.
Aidha, nchi zisizo na silaha za nyuklia zilianzisha mazungumzo hayo na kuelezea kuongezeka kwa hali ya tatizo hilo kwamba juhudi za kutokomeza silaha za nyuklia zimekwama.
Marekani, Urusi na nchi nyingine zenye nguvu za nyuklia, pamoja na zile zinazotegemea nyuklia, kama Japani na mataifa mengi ya Umoja wa Kujihami wa nchi za Magharibi - NATO, hazikushiriki katika mazungumzo hayo, zikidai kuwa mkataba wa utokomezaji wa silaha hizo hautofikia suluhisho linaloweza kutekelezeka.
Wajumbe hao wanajadiliana juu ya rasimu ya mkataba uliowasilishwa na mjumbe kutoka Costa Rica, Elayne Whyte Gomez, ambaye ni mwenyekiti wa kikao hicho. Wanapanga kupitisha vifungu vya mkataba huo ifikapo Julai 7, siku ya mwisho ya mazungumzo hayo.
Utangulizi wa rasimu hiyo unarejelea mateso ya Hibakusha, au waathirika wa silaha za nyuklia, na kudai kwamba silaha za nyuklia zinakiuka sheria za kimataifa za haki za kibinadamu.
0 Comments:
Post a Comment