Ni taarifa ya chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema ya
kuwafukuza uanachama viongozi wake wawili ambao kwa mujibu wa chama hicho
walikwenda kinyume cha kanuni na taratibu za chama hicho.
Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Arusha Mh. Amani Golugwa (Katikati) Picha ya V.O.A TV |
Katika kikao cha Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Arusha na
katibu wa Chama hicho kanda ya kaskazini Bw. Amani Golugwa na waandishi wa
habari katika makao makuu ya chama hicho Arumeru Mashariki amethibitisha
uhalali wa kufutwa uananchama na dhamana ya uongozi waliyopata kupitia Chadema.
Mh. Golugwa amesema Chama hicho ni chama makini katika
utendaji na utekelezaji wa majukumu yake katika jamii yenye uhitaji. Amesema
chama hicho hakitamvumilia mwanachama yeyote atakayekwenda toauti na kanuni ,
taratibu na katiba ya chama hicho. “Ni Bora kuwa na watu wa chache kuliko kuwa
na watu wengi wanafiki” Mh. Golugwa.
Kabla ya kikao hicho rasmi ya Chadema kulikuwa na tetesi
kuwa Diwani wa wake amejiuzulu tetesi ambazo zilishika kasi hasakatika mitandao
ya kijamii. Kikao hicho kilikuwa na lengo la kuweka wazi hali hiyo ya
sintofahamu iliyokuwa ikiendelea na chama hicho Arumeru.
Bw. Golugwa anasema “
Tuna shauri inayomuhusu Ndugu Emanuel Mollel diwani wetu katika kata ya Makiba
na Josephine Anaeli diwani wetu wa viti maalumu , siku za hivi karibuni
kumekuwa na uvumi katika mitandao ya kijamii kwamba Ndugu Emanuel Mollel
amejiuzulu ambapo ofisi yetu ya chama
Arumeru Mashariki ikapokea barua ya Ndugu Emanuel Mollel akijieleza kwamba
anaomba kujiuzulu na kujivua uanachama baada yak kupokea barua ile kamati yetu
tendaji ya chama ikakutana. Tuligundua mapungufu makubwa katika barua ile pungufu kubwa lilikuwa lile barua
halijasainiwa na haikuwa imewekwa tarehe ya kuandikwa chama kikatumia hekima ya
kumuandikia barua ndugu Emanuel nakuthibithisha kwa maneno yake kuwa
amejiuzulu” Alisema Mh. Golugwa
Katika hatua nyingine chama hicho kupitia Kiongozi wake huyo
wa ngazi za juu ilitoa ufafanuzi juu ya Aliyekuwa Diwani wa viti Maalum wa
Chama hicho Ndugu Josephine Anaeli kwamba pamoja na tetesi kuwa huenda akafutwa
uanacha au kuvuliwa uanachama amesema Ndugua Josephine amekuwa akibadilika siku
hadi siku ikiwa ni pamoja na kwenda kinyume na madiwani wengine na kwamba
amekuwa akionesha kila dalili za uzembe katika kushughulikia masuala mbalimbali
ya wananchi. Kiongozi huyo wa ngazi za juu wa Chadema ameeleza kuwa kama
viongozi wa chama Mkoa wamekuwa wakipata malalamiko mara kadhaa kuhusiana na
Ndugu Josephine na Emanuel Mollel ambao wote wamekuwa vibaraka wa kukiuza chama
hicho kwa kushirikiana na chama cha mapinduzi.
Viongozi mablimbali wa chama hicho Arumeru Mashariki pamoja naMwenyekiti wa Chama hicho mkoa wa Arusha na katibu Kanda ya kaskazini Mh. Amani Golugwa. Picha ya V.O.TV |
Ni Utaratibu uliozoeleka kuwa kiongozi lazima awe
amejitosheleza kiasi cha asiwe ombaomba Bw. Golugwa amesema Ndugu Emanuel
Mollel amekuwa akikopa huku na kule na kuonekana katika ameneo mabalimbali
ambayo chama ingemtilia shaka hasa kwa kuwa na ushirikiano na viongozi teule wa
serikali ya chama tawala.
Mh. Golugwa ameeleza kwa kabla ya kufika hatua ya Diwani
huyo Ndugu Eamanuel kutaka kujiuzulu amekuwa akituhumiwa na chama kwa
kutoshiriki ipasavyo katika majukumi ya kiutendaji hasa kusimamia miradi ya
maendeleo , kushiriki vikao, na kutotoa taarifa za kiutendajia mambo ambayo
alishindwa kutekeleza na hatimaye kuamua kujiuzulu.
“kwa mujibu wa Ibara ya Chadema 5;4;1 mwanachama anaweza
kukoma unachama kwa hiari yake. Kabla Chama kilimtaka Ndugu Emanuel kujibu
tuhuma zilizomkabili , Amekuwa akituhumiwa kwa kutosimamia miradi na kutotoa
taarifa za kimaendeleo”
Nimekuwekea Full video kutoka V.O.A TV bomyezakitufe cha play kuona alichosema Mh. Golugwa
Aidha katika mazungumzo Zaidi Bw. Golugwa amefafanua
kuhusiana na taarifa za chama hicho kumtuhumu Diwani wa Viti maalum Ndugu
Josephine Anaeli “Tumepokea nakala ya barua yake barua yake aliandika kwa
mkurugenzi na nakalaikaenda kwa Mwenyekiti wa halmashauri na nakala nyingine
imekuja kwa katibu wa chama Wilaya kama mamlaka ambayo imedhamini fomu zake ,
baada ya kupokea nakala zile tumemtafuta kwa jitihada zote kwa njia ya simu ,
barua kwa kupiga simu kwa ujumbe mfupi amekuwa hajibu , hata kikao cha leo
ametaarifiwa ili aje ajieleze ajibu maswali kuwa nini kimetokea Bi Josephine
amegoma na amekataa kuitikia wito.” Aliongeza Mh. Golugwaa
“ Bi. Josephine amekuwa akituhumiwa kwa kusababisha migogoro
mingi sana ndani ya Chama cha ajabu sana amekuwa akigombana na madiwani wenzake
amegombana sana na wanawake wenzake kama nilivyosema huyu amekuwa katibu wa wanawake kwenye jimbo letu la
Arumeru , amekuwa akigombana na mwenyekiti wake wa BAWACHA Bi. Rebeca Ngoro
aliyekuwa Mbunge wetu wa Arusha , amekuwa na tabia za kijinga jinga , tabia za
kitototo tabia za kipuuzi” Bw. Golugwa
anasema baaada ya hapo wamekuwa wakimuandikia barua kujibu kwa nini amekuwa
akisababisha uchonganishi.
Mbali na hayo ni kwamba chama kimekuwa kikipata Malalamiko
kufuatia Diwani huyo wa viti maalumu kutoshiriki kikamilifu katika utendaji na
utekelezaji wa majukumu ya umma. Ambapo Bi. Josephine amekuwakichelewa kufika
katika vikao au kuwahi kutoka na masuala mengine.
“Kuhusiana na Ndugu Emanuel Mollel ni kwamba amekuwa natabia
ya kuombaomba , kukopa kopa kuzidi uwezo wake “ Bw. Golugwa amefafanua katiba
ya chadema ukurasa wa 124 sehemu ya sita kiongozi anatarajiwa kujitosheleza
yeye na familia yake kwa mapato halali na kuepukana na tabia ya kukopa kwa
kuzidi uwezo wake au kuwa ombaomba kwani tabia hii itathoofisha uwezo wake wa
kutoa maamuzi sahihi bila ya upendeleo .
Hata hivyo katika kuhitimisha Mh. Golugwa Mwenyekiti wa
Chadema Mkoa wa Arusha na Katibu wa Chama hicho kanda ya Kaskazini amesema
vikao vya chama hicho vitaendelea kuketi mapema kujadili na kulitolea maamuzi
suala la uanachama wa Bi. Josephine kwa kushindwa kuzijibu tuhuma zinazomkabili
dhidi ya chama.
Rasmi Chama hicho kimemfuta uanachama na kumvua dahama na
udiwani ikiwa ni pamoja na mambo yote aliyowahi kuyafanya akiwa mwanachama na
diwani kupitia chama hicho Ndugu Eamanuel Mollel. Huku uamuzi kuhusu Bi.
Josephine ukiwa bado utasubiriwa kwa kamati ya chama hicho ambacho kitakutana
mapema na kulitolea uamuzi kama iwapo Bi. Josephine atatimuliwa uanachama au
la!.
No comments:
Post a Comment