Thursday, June 15, 2017

EXCLUSIVE: DC Hai adaiwa kumsababishia Mbowe hasara ya Millioni 530

Siku   moja baaada ya mkuu wa  wilaya ya Hai Gelasius Byakanwa kuivamia shamba la Mwenyekiti wa Chama cha Demkrasia na Maendeleo (Chadema) Taifa Freema Mbowe akiwa na baraza la uisalama la wilaya  uongozi wa chama cha demkrasia na maendeleo (CHADEMA) , Meya wa halmashauri ya jiji la Arusha Mh. Kalisti Lazaro , Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema wameitembelea shamba hilo na kujionea uharibifu mkubwa uliotekelezwa na Mkuu wa wilaya ya Hai Gellasius Byakamwa.

Chama hicho kiliongozwa na katibu wake mkuu wa Kanda ya Kaskazini Mh. Amani Golugwa.
Katibu mkuu wa CHADEMA  Kanda ya Kaskazini Mh. Amani Golugwa , Kushoto ni Mbunge wa Arusha Mjini Mh. Godbless Lema wakikagua tents zilizoharibiwa vibaya  katika shamba la mwenyekiti wa chama cha demkrasia na maendeleo taifa Mh. Freeman Mbowe. Picha ya V.O.A TV

Awali Wakizungumza na Habaritanzaniagracemacha.com na V.O.A TV baadhi ya wazee wa kimila , na wenyeji wa maeneo hayo waimbia V.O.A TV kuwa wao kama wazawa wa eneo hilio walilifahamu tanguwakiwa wadogo ambapo shughuli za kilimo zilikuwa zikiendelea katika zaidi ya milongo kadhaa hadi hivisasa na hawakuwahi kushuhudia kitendo cha namna mkuu wa wilaya hiyo alivyovamia na kufanya uharibifu mkubwa wa miundombinu na chakula.

Msimamzi wa Bustani huyu hapa bofya play. VIDEO BY V.O.A TV  


Wazee hao ambao walionekana kuumizwa na kukguswa na suala hilo wamelaani vikali suala hilo huku wakisisitiza kuwa kwa taratibu za mila ya jamii ya eneo hilo la Kichaga kitendo hicho ni sawa na mauaji ya halaiki.  kuharibu miundombinu ya shamba hilo ambalo huwalisha wakazi karibu wote wa maeneo hayo kunapelekea zaidi ya wakazi 10000 kukosa huduma ya chakula hasa mboga , matunda na hata ajira.

Shamba hilo la lililokuwa likiendeshwa kwa kilimo cha kisasa cha Green House irrigation kitaalamu limekuwa limekuwa likiajiri wafanyakazi zaidi ya 100 huku aikilisha wakazi wote wa eneo Machame, Boma Ng'ombe , moshi na hata maeneo mengine ikiwemo jijini Dar Es salaam. 
V.O.A TV iliwakuta wafanyakazi waliokuwa wakifanyakazikatika shamba hilo wakiwa katika huzuni kubwa ya huku wakilalamika watakula wapi?

Mzee  Kalebi Emanuel Nkya ameeleza " Nimezaliwa 1935 wakati  tulikuwa  tnasoma tulikuwa tunaenda kwenye ziwa karibu na mto weruweru tunaenda kuoga , migomba ilikuwa hapa ndizikiiva huwa tunatingisha mti nakuzila , kulikuwa na kilimo cha migombana mboga mboga na hakukuwa na shaka" 
"Katika mila yetu sheria ya mchaga hata kama mtu amelima shamba lako ameshalima mahindi yamebeba huwezi kukata chakula unaenda kushtaki , kukata mgomba wa kichaga kwa hasira na sawa na mauaji, huyo mtu alikuja kuvunja vunja chakula ni kama ameua" alisema mzee Kalebi Emanuel Nkya


Naye Mzee Bartholomew Mbowe ambaye pia ni mwenyekiti wa Mazingira Machame aliyezaliwa mwaka 1940 anasema "kwanza mimi ni mwenyekiti wa mazingira tangu mwaka 2003 , sijawahi kuona jambo kama hili la jana" , Mbowe alitusaidia sana alitupa miti kila mtu alimpatia mit kumi ili azipande tukaziotesha. Jana nimeona kitu cha ajabu yaaniwachaga wote tumekufa, hili eneo limekuwa likitusaidia sana tumepata elimu hapa , tunategemea sehemu hii kwa chakula na ajira kwa waoto wetu badala ya kwenda kutumiamadawa ya kulevya" mzee huyu anahoji je huu ni ubaguzi? huku akisisitiza kuwa suala hilo ni mauaji kama walivyoeleza wazee wengine. Video hii hapa chini Bonyeza 

Kwa upande wa mzee huyu Penanieli Swai anasema amefanyakazi kwa zaidi ya miaka 30 huku akikukbuka jinsi Mh. Freeman Bowe alivyojituma katika kuyajenga na kuyatunza mazingira kwa kupanda miti maeneo mbalimbali na kuyakuza katika hali ngumu "Tulikuwa tunalima hapa , mboga tunauza hapa wananchi wamekuwa wakija hapa na kununua hapa , baadaye tukamuomba mheshimiwa atufanyie eneo hilo liwe kisasa. akatuletea hayo Green house, na hakuna uaharibifu wowote wa mazingira hapo kwani hakuna maji yanayoelekea mtoni maji yote hishia kwenye green house, sasa jana tulishangaa mkuu wa wilaya amekuja hapa ametuharibiashamba letu hatujui hata tutaenda wapi" Alisema mzee Penanieli Swai  Play Video iko hapa chini 

Eneo hilo limekuwa na heshima kubwa kwa jamii nzima hapo kwani watu wengi wamepata elimu kuhusu kilimo cha kisasa cha umwagiliaji Mzee Emanuel Mbowe anasema "Hii bustani ni ya asali hapa mimi nimezaliwa 1934 tangu wakati huyo tumekuwa hapa hadi tunakua baba zetu wamelima hapa na sisi tumelima hapa hakuna tatizo , kulikuwa na Migomba kulikuwa na kahawa , baadaye tukamuomba mbunge wetu atusaidie kuboresha eneo hilo , uongozi kama umeshakuwa wa nguvu hivyo basi bwana ." Mzee Emanuel Alieleaza huku akinesha ghadabu kubwa aliyonayo. Play Video Hapa Chini

katika kuwatafuta wenyeji zaidi wa eneo hili V.O.A TV ikampata Mwenezi wa CHADEMA Wilaya Bw. Nasoro Mushi ambaye amlitaza suala hili kwa jicho la tatu kuwa kimsingi sehemu kama hiyo mkuu wa wilaya angeitisha mazungumzo juu ya jambo hili "Kichaga tatizo linapotokea haiwezekani kakatwa mahindi amabye yamesha ota , Kitendo cha jana cha mkuu wa wilaya mimi ndhani mkuu wa wilaya anagekuja kama baba nakulisimamia suala hili kwamazungumzo , siyo kuja na mapanga,  bunduki , na nyundo. akamlizia kwa kuhoji kuwa hata nyanya unaijia na Bunduki? Zaidi nimekuwekea video hapa 

Katibu wa kanda ya kaskazini wa CHADEMA Mh. Amani Golugwa  amesema "Formula ambayo watawala wanaitumia au wametaka kuitumia ni mpige mchungaji kondoo watatawanyike wanamdhoofisha mwenyekiti wetu wamemuingilia katika bishara yake halali wakifikiri na wakidhani watamudhoofisha , hiki walichokifanya waingia chumbani sasa tumeshaijua mienendo ya awamu hii ya tano,  watu wote waliokuwa wakifanya kazi hapa wameharibiwa kazi zao , hatutakubali ushetani kama huu ufanyike katika mkoa wetu wa kilimanjaro" Alisema Golugwa

Aidha Meya wa Jiji la Arusha amesema kitendo hicho alichokifanya mkuu wa wilaya ni sawa na mauaji "Kitendo hicho ni sawa na mtu amefika nyumbani kwako nakufanya mauaji akaua watoto akaua mke wako akua mifugo yako yote, wamuua Mbowe ,wameiua familia yake, mbowe wakati wa akiwa mbunge aliyepanda miti kwa zaidi yakilomita 60 , miti aliyopanda ni zaidi ya 3000000 , kwa mila ya kiafrika mkuu wa wilaya anastahili kushtakiwa kwa kosa la mauaj " Mstahiki Meya alimtaka Mwenyekiti Mbowe awe mvumilivu.  Zaidi ni kwenye Video ambayo nimeiweka hapa tayari.

Kwaupande wake Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Mh. Godbless Lema amelezea suala hilo kama kumdhoofisha mwenyekiti wa Chadema huku akihoji kama kusudi ni umbali kutokachanzo cha maji kama ilivyokuwa madai ya NEMC mbona kuna taasisi za serikali ambazo zimejenga pembezni mwa mito? maeneo hayo ni Pamoja na TRA Arusha , Sea Clief hoteliko baharini , Koro beach ipo baharini , coco beach iko baharini hilton hotel iko baharini na jengo la Chama cha mapinduzi Sanawari lipo mtoni.je lipi ilikuwa ni hatari je ni hili la Green house? 


Mkuu wa wilaya ya Hai Bw. Mh. Gellasius Byakamwa. akitekeleza suala kuharibu mindo mbinu ya shamba la M/Kiti wa Chadema Mh. Freeman Mbowe. Picha ya Maktaba.

akieleza sababu za kuvunja vunja na kuharibu shambahilo mkuu wa wilaya Bw. Mh. Gellasius Byakamwa Amesema anatkeleza sheria inayosema ni marufuku kujenga kando ya ya mto kwa umbali usiochini ya Mita 60 klipo chanzo cha maji.

Bw. Frank Charles Ni mwanafamilia wa Mh. Mbowe anaeleza jinsi suala hilo lilivyofanyikana taratibu ambazo zingefuatawa "Hili shamba limekuwa hapa kwa zaidi ya miaka 80 , wakati wa enzi za Mwl, Nyerere Kilimo kilihamasihwa sana katika mkoa wa Kilimanjaro ambapo jitihada zilikuwa zinashindwa kwa sababu ya uhaba wa ardhi ya kilimo, Eneo hili siyo chanzo cha maji tangu enzi za mababu zetu maji yanatoka zaidi ya maili moja yanapita sisi ndo  tunatunza huu mto na kwa sababu hiyo hata wawekezaji wanaotumia maji haya wanakuwa hawakosi maji kwa sababu ya utunzaji tunaoufanya sisi. hili lingekuwa jambo la kutufariji siyo la kutuvunja moyo "Alisema Frank Charles 

Mali iliyoharibiwa na makadirio ya gharama zake
1. Tents 29 (Zote zimeharibiwa) Tent moja hugharibu  Tsh. 18,000,000 . Jumla ya gharama ya tents zote ni Tsh. 522,000,000
2. Pipes za maji kubwa zilizoharibiwa 29 gharama yake jumla ni 1,392,000
3. Pipes za maji ndogo mizunguko 3 gharama 4,050,000
4. Plastic Mulch yakuweka juu ya udongo 3 gharama zake 2400000 
5. Valves 16 gharama zake 892,000
kampuni ya kilimanjaro Virggies imeingia hasara ya jumla ya Tsh. zaidi ya 530,734,000/=
takwimu hizi ni kwa mijibu wa V.O.A TV na Habaritanzaniagracemacha.com

No comments:

Post a Comment