Wednesday, June 7, 2017

BURUDANI: Ali Kiba ampongeza Diamond Platnumz

Ali Kiba amesema Diamond hakuwahi kuwa mshkaji wake. Akiongea katika kipindi cha Mikasi  Channel 5 Jumatatu usiku, Kiba akasema alikuwa akimchukulia Diamond kama mdogo wake. “Mimi nilikuwa rafiki na dadake Diamond – Queen Darleen, hivyo kwangu mimi Diamond alikuwa kama mdogo wangu na yeye alikuwa akiniita kaka. Na mimi ndiye niliyetoa idhini wimbo wake “Kamwambie” urekodiwe kwa Bob Junior, nilikuwa nipo kwenye kebineti ya studio za Sharobaro hivyo kila kinachofanyika ilikuwa lazima Bob Junior anishirikishe.

Kipindi hicho nilikuwa Marekani, Bob Junior akanipigia simu kuhusu Diamond, nikamwambia kama anajua kuimba basi mpe nafasi ya kurekodi.” Aidha, Kiba amesema hapendi watu wanavyojaribu kumfananisha au kumlinganisha na Diamond kwani yeye anamchukulia msanii huyo kama wasanii wengine walivyo.

Kiba anaeleza zaidi: “Mara kadhaa Diamond katika siku za nyuma alikuwa akipenda kuzungumzia suala la kunifunika, nadhani alininuwia kwa muda mrefu, lakini mimi namchukulia kama mdogo wangu.” Pamoja na hayo, Kiba alisema anampongeza Diamond kwa mafanikio kibao aliyonayo katika ngazi za kimataifa ikiwemo kuingizwa kwenye tuzo kadhaa kubwa barani Afrika na duniani kwa ujumla..... " Ali Kiba - Samisago..

No comments:

Post a Comment