KAMATI YA ULINZI NA USALAMA YA WILAYA YA HAI IKIONGOZWA NA MKUU WA WILAYA WAVAMIA SHAMBA LA MBUNGE WA HAI LILILOKO NYUMBANI KWAKE MACHAME NAKUHARIBU MIUNDO MBINU NA MALI PAMOJA NA MBOGA NA MIMEA MBALIMBALI.
Shamba La Mbowe Lavamiwa
Kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya ya Hai ikiongozwa na mkuu wa wilaya hiyo, Gellasius Byakanwa wamevamia shamba la mbunge wa jimbo hilo, zMh. Freeman Mbowe lililoko nyumbani kwake Machame na kuharibu miundo mbinu na mali pamoja na mboga mboga na mimea.
Mh. Mbowe amezungumza na Jahazi moja kwa moja kutoka bungeni mjini Dodoma... "Ni kweli nimezipata hizi habari mkuu wetu wa wilaya akiambatana na askari na waandishi wa habari walikwenda kwenye mradi wetu na kukatakata mimea na kufanya uharibifu mkubwa, taarifa nilizozipata kutoka kwa wafanyakazi waliopo site walisema walipokea barua kutoka NEMC kuwa kilimo tunachokifanya kinaharibu mazingira na hatukustahili kuendelea na kilimo kile, ni jambo la kufedhesha sana tunawahamasisha watanzania wawekeze kwenye kilimo cha kisasa lakini viongozi wa serikali bila kuheshimiana wanakwenda kuharibu, sio kweli kilimo chetu hakiharibu mazingira, familia yetu imelima kwenye shamba hilo kwa zaidi ya miaka 80"
Picha za Muonekano wa shamba hilo baada ya kuharibiwa vibaya. Picha ya V.O.A TV |

0 Comments:
Post a Comment