KATIBU Mwenezi wa Baraza la Vijana CHADEMA, (BAVICHA), Taifa, Edward Simbeye amesema kuanzia sasa watashughulika na yoyote atakayejaribu kumuonea na kumnyanyasa Mwenyekiti wa Taifa wa Chama hicho, Freeman Mbowe.
Aidha, Waziri Mstaafu, Frederick Sumaye, amesema siasa za chuki na visasi ni siasa chafu haitaiacha nchi salama huku akilaani vitendo vya uonevu anavyofanyiwa Mbowe.
Waliyasema hayo jana wakati wakiongea kwenye mahafali ya Jumuiya ya wanafunzi wa Chadema Vyuo Vikuu, (CHASO), mkoani Arusha ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu Mstaafu, Sumaye.
Simbeye alisema kuwa wamwekuwa kimya kwa mambo aliyokuwa akifanyiwa Mbowe siku za nyuma kwani walikuwa wanajua ni siasa na yataisha ila kwa sasa wameona yanayoendelea yanahatarisha usalama wa maisha ya kiongozi wao.
Alisema kuwa wanajivunia kuwa na kiongozi huyo ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi Rasmi Bungeni, (KUB) aliyedai kuwa ameonyesha misimamo isiyoumba katika kupigania haki, usawa na demokrasia nchini na anayefanya kazi hiyo bila kulipwa chochote hivyo watamlinda kwa gharama yoyote.
"Mbowe ni kiongozi shupavu wa kupigania haki mwenye msimamo usioyumba, wamemharibia biashara zake, wamemsingizia kashfa mbalimbali sisi tulikuwa kimya tuliona ni siasa tu zitaisha lakini hapa walipofika wanahatarisha usalama wa kiongozi wetu" alisema Simbeye na kuongeza.
"Sasa sisi vijana wa Chadema tumesema basi imetosha, Bavicha hatutakubali kuona Mwenyekiti wetu anaonewa tena, tutapambana na yeyote, wakati wowote, muda wowote iwe mchana iwe usiku kwa gharama yoyote kumlinda Mwenyekiti wetu.
Tunahitaji kuonyesha nafasi yetu kama vijana ndani ya chama chetu, siasa zilipofikia wasambaa wanasema kama mbwai na iwe mbwai,"
Sasa sisi vijana wa Chadema tumesema basi imetosha hatutakubali kuona mwenyekiti wetu akionewa na kunyanyaswa,".
Kwa upande wake Waziri Mkuu Mstaafu, Sumaye ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema alisema kuwa siasa za chuki ambazo zimekuwa zikiendelea kuwaumiza wafuasi na upinzani pamoja na viongozi wake hazitaiacha nchi salama.
"Hii ni siasa chafu, haitaiacha nchi salama, unaharibu mali za watu kwa kuwa yuko upinzani, unafunga biashara ya mtu kwa kuwa unadhani anausaidia upinzani, msilipe kisasi hata Mungu alisema kisasi ni tumuachie yeye. Kisasi ukianza kukitekeleza kwa vyovyote kitakurudia wewe na watoto wako na wajukuu zako, naharibu mali za wenzako? ," alisema Sumaye.
Alisema kuwa mashamba ya Mbowe yaliyoharibiwa ndiyo alikuwa yanasambaza mboga kwenye maduka makubwa (supermarket) za jiji la Dar es Salaam jambo alilodai kuwa maduka hayo yataathiriwa na tukio hilo kwa namna moja au nyingine.
" Unajiuliza Dc tangu lini kawa mtekelezaji wa NEMC (baraza la usimamizi wa Mazingira nchini) mpaka aende akaharibu miundo mbinu na mboga shambani, shamba hilo lipo tokea enzi za Aikael Mbowe, sasa unajiuliza shamba limefuata mto au mto umefuata shamba? Mto ule umenzia mlimani wao wanasema lipo kwenye chanzo cha maji, chanzo gani kinakuwa katikati ya mto?," alihoji Sumaye.
Aliwaonya viongozi vijana aliodai kuwa wanafanya visasi ajili ya kuwapendeza watu watawaacha jangwani watakuwa wenyewe wataona cha mtema kuni.
"Huwezi kwenda kukata mali ya mtu unapeleka mgambo na mapanga wanakata mazao na miundombinu. Afadhali wangesema shamba hili tunalitaifisha liendelee kuhudumia wananchi,"
Alisema hata wakati wa mwalimu Julius Nyerere alipotaifisha mashamba makubwa yaliyokuwa yakimilikiwa na wageni hakiyaharibu kwa kupitisha greda Bali aliyarejesha kwa wananchi yaendeleze hivyo akashangazwa kwa vitendo hivyo vilivyofanywa na mkuu wa Wilaya ya Hai.
"Siasa ya visasi haimwachi mtu salama, hawa vijana wanaojifanya wana damu ya moto itapoa,hamuwezi kuwa mnatesa watu kwa sababu tu mmepewa nafasi kwanza hawa wanaofanya hivyo wanaonyesha hawastahili hizo nafasi, wanaostahili hawawezi kufanya mambo ya kijinga.
"CHADEMA itaingia madarakani 2020, upuuzi na ujinga wote utakoma na ndipo Watanzania wataanza kufurahia matunda ya vyama vingi vya siasa,"
Aliwataka wahitimu hao wasiogope changamoto watakazokumbana nazo pindi wakirudi uraiani kwani hakuna kisichokuwa na mwisho huku akitolea mfano kuwa utawala Roma uliangushwa jambo alilohoji sembuse CCM?.
Mbowe ambaye ni Mbunge wa jimbo la Hai mwaka uliopita aliondolewa kwenye jengo alilokuwa akiliendesha kwa ubia na shirika la Nyumba la Taifa, (NHC) ambapo vifaa vilivyokuwa ndani ya jengo hilo viliharibiwa wakati vikihamishwa na kampuni ya udalali iliyofanya hayo kwa maelekezo ya NHC ambapo zoezi hilo lilihitimishwa kwa jengo hilo kubomolewa.
Aidha kiongozi huyo alitajwa kwenye orodha ya watu wanaodaiwa kufanya biashara ya dawa za kulevya kabla ya hivi karibuni Mkuu wa Wilaya ya Hai, Gellasius Byakanwa, kuongoza kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo kuvamia shamba lake na kuharibu mazao na miundo mbinu.
Mpaka sasa hasara iliyotokana na uvamizi huo wa Mkuu wa Wilaya inakadiriwa kufikia zaidi ya shilingi milioni 500 kwani shamba hilo lilikuwa linaendesha kilimo cha kisasa na kitaalam cha mbogamboga na migomba.
Viongozi wengine waliohudhuria kwenye mahafali hayo ni pamoja na mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, Naibu Meya wa jiji la Arusha, Viola Likindikoki, Mwenyekiti wa Chadema.

0 Comments:
Post a Comment