UPDATES: Kutoka Dodoma Nimekusogezea alichoongea Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe

Mwenyekiti wa CHADEMA Mh. Freeman Mbowe 


Anachosema Mh. MBOWE kuhusu Uwekezaji nchini.

"Tusikimbilie kumtukana anaetuibia, tumemtengenezea utaratibu atuibie alafu tunapiga kelele.
Tunahitaji marekebisho makubwa ya sheria zetu ili kuondoa mianya hii"

"Sisi CHADEMA tunaamini kwamba utaratibu unaotumika na Rais katika kushughulika na hili swala litatupelekea kama taifa kushitakiwa katika mahakama za kimataifa na uwezekano mkubwa wa kushindwa kesi hizo upo na kupigwa faini za mabilioni ya pesa.
Ni muhimu kama taifa kuwa makini sana tunapofanya maamuzi juu ya wawekezaji."


Pamoja na yote yanayojiri ni kwamba mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Atoa kauli rasmi ya chama hicho kuhusu uchaguzi wa Kenya

 "Nimalizie kwa kuzungumzia uchaguzi unaotarajia kufanyika nchini Kenya.
Kwa muda mrefu chama chetu kimekuwa kikimuunga mkono Raila Odinga achukue nafasi ya kuliongoza taifa hilo.
Mwaka 2015 ilipofika zamu yetu, rafiki wetu huyu alitugeuka na kumuunga mkono adui yetu.
Hivyo sisi kama chama, safari hii tunamuunga mkono Rais Kenyatta na umoja wa vyama vinavyounda JUBILEE" Mh. MBOWE

Sasa rasmi CHADEMA wamuunga mkono Kenyatta Uchaguzi Kenya

0 Comments:

Post a Comment