Sunday, May 7, 2017

UPDATES, TAARIFA: UMOJA WA VYUO VYA UANDISHI WA HABARI TANZANIA SALAMU ZA POLE KWA WAHANGA WA AJALI ILIYOONDOA MAISHA YA WATU 32 - ARUSHA


                                "TAARIFA KWA UMMA

"Umoja wa vyuo Vya Uandishi wa habari Tanzania kupitia vyuo vya uandishi wa habari , Uongozi wa Vyuo , Serikali za wanafunzi pamoja na wanafunzi wote tunaungana na Watanzania wenzetu kwa kuwapa Pole Wazazi, Ndugu, jamaa, marafiki na Uongozi Mzima wa Mkoa wa Arusha kupitia Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bw. Mrisho Gambo

Tumepokea kwa Mshtuko na masikitiko makubwa taarifa ya vifo vya wanafunzi 32 wa Darasa la saba , walimu 2 na dereva wa gali la shule ya msingi iitwayo Lucky Vicent Mkoa wa Arusha vilivyotokea leo Tarehe 06 May , 2017 Saa 3 Asubuhi Baada ya Gari walilokuwa wakisafiri kupata ajali katika eneo Rhotia marera, Wilaya ya Karatu Mkoani Arusha.


No automatic alt text available.
Msiba huu ni mkubwa Umeugusa Taifa letu letu.

Nakala kwa: Vyuo Vyote vya uandishi wa habari nchini Tanzania na wamiliki wa vyombo vya habari(MOAT)
Mwenyekiti wa Umoja wa Vyuo Vya Uandishi wa habari Bw. Michael Charles Chali

Imetolewa na
Michael Charles Chali
Mwenyekiti wa Umoja wa Vyuo Vya Uandishi wa habari,
Dar-es-salaam,Tanzania,
06 May , 2017."

No comments:

Post a Comment