Tuesday, May 30, 2017

MASHARIKI YA KATI: IRAN KUHUSU UVAMIZI WA ISRAELI PALESTINA


Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza juu ya kuendelezwa muqawama na mapamrbano dhidi ya uvamizi wa utawala ghasibu wa Israel.
Bahram Qassemi amesema hayo leo katika mkutano wake na waandishi wa habari wa ndani na nje ya nchi na kueleza kuwa, msimamo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mkabala na uvamizi wa utawala ghasibu wa Israel si wenye kubadilika na kwamba, madhali uvamizi wa Israel unaendelea, mapambano na muqawama dhidi ya Wazayuni maghasibu nao utaendelea.
Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amezungumzia safari ya hivi karibuni ya Rais Donald Trump wa Marekani huko nchini Saudi Arabia na kukaririwa madai yasiyo na msingi dhidi ya Iran na kusema kuwa, safari ya Trump katika nchi ambayo ni eneo salama la ugaidi na madai yake ya kupambana na ugaidi ni batili na yasiyokubalika.

Bahram Qassemi, Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran 

Bahram Qassemi amesema kuwa, matamshi ya Rais wa Marekani hayan maana na ni batili na kuongeza kuwa, kuituhumu Iran kwamba, inaunga mkono ugaidi ni matamshi ambayo kimsingi hayakubaliki hata kidogo.
Aidha Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amezungumzia matukio ya kieneo kwa ujumla na kubainisha kwamba, sera za madola makubwa katika Mashariki ya Kati hakuna wakati ambao zilikuwa na msaada katika urafiki.

No comments:

Post a Comment