Tuesday, May 2, 2017

KIMATAIFA; Rais Trump asema yupo tayari kufanya mkutano na Kim Jong Un

Ndege za kuangusha mabomu aina ya B-1B Lancer zikipaa juu ya Korea Kusini awali
NDEGE ZA MAREKANI
Rais wa Marekani Donald Trump ameelezea utayari wake wa kukutana na Kiongozi Mkuu wa Korea Kaskazini Kim Jong Un katika wakati muafaka. Katika mahojiano na shirika la habari la Bloomberg jana Jumatatu, Rais Trump alisema kuwa itakuwa heshima kukutana na Kim Jong Un.

Maoni hayo yanachukuliwa kama nia ya kutaka kuonesha kuwa Rais Trump bado hajaondoa uwezekano wa kufanya majadiliano na Kim Jong Un, huku akiendelea kuishinikiza Korea Kaskazini iachane na mipango yake ya uendelezaji wa nyuklia na makombora.

Msemaji wa Ikulu ya Marekani, Sean Spicer aliwaambia waandishi wa habari kuwa iwapo Korea Kaskazini itaonesha nia ya dhati ya kuharibu uwezo wake wa nyuklia na kuondoa tishio kwa eneo hilo pamoja na Marekani, kutakuwepo na uwezekano wa kufanya mkutano huo.

Spicer alisema ikiwa Korea Kaskazini itaendelea kutekeleza vitendo vya kichokozi, mazingira muafaka kwa ajili ya mkutano huo hayatafikiwa.

No comments:

Post a Comment