Friday, May 26, 2017

HIVI PUNDE: Mill. 35 zatolewa kwa vikundi saba Arusha.

Mkurugenzi wa ARUSHA VICOBA IMPOWERMENT Bi. Grace Macha (kushoto) katika hafla ya kukabidhi fedha za mikopo kwa vikundi saba leo katika kata ya Levolosi

Ni katika kuiniua maendeleo ya wananchi hususan kwa vijana na kina mama kupitia vikundi yaani (VICOBA).
PLAY VIDEO HAPA AKIZUNGIMZA BI. GRACE MACHA MKURUGENZI WA ARUSHA VICOBA IMPOWERMENT

Serikali imetoa  IMETOA 35 MILL. Kwa ajili ya kuiniua uchumi wa vijana na akina mama. Fedha hizo zimekabidhiwa kwa Kampuni ya Arusha Vicoba Empowerment. Ili kuweza kupewa vikundi mbalimbali vya Saccoss .

Akizungumza wakati ya shughuli ya ukabidhi wa fedha hizo Mkurugenzi wa ARUSHA VICOBA IMPOWERMENT Bi. Grace Macha amesema fedha hizo no kwa ajili ya kuiniua halo ya kiuchumi na maendeleo kwa ujumla na kuwataka wanaopewa fedha hizo za mikopo wazitumie ipasavyo ili fedha za seikali zisipotee.

"Fedha hizi tunazitoa kwa malengo husika zitumike ipasavyo , endapo PESA zitatumika vinginevyo na mkashindwa kurejesha tutawatafuta popote mlipo ili fedha za serikali zitumike kwa makusudi yaliyowekwa" Mkurugenzi wa ARUSHA VICOBA IMPOWERMENT Bi. Grace Macha.

Katika hatua nyingine Mwenyekiti wa ARUSHA VICOBA IMPOWERMENT Bw.  Hassan Moses  Ameiomba serikali kuwapa ushirikiano zaidi ili waweze kuwahudumia wananchi katika kata zingine ambapo leo no kata ya Levolosi ndiyo waliopata Mikopo hiyo.
Vikundi vilivyokabidhiwa fedha za Mikopo leo
Naye Mtendaji wa Kata Levolosi Bi. Esta  amesisitiza kuwa vijana kuanzia miaka 15+ wanauwezo wa kupata mikopo hiyo wakiwa katika vikundi vya kijasiriamali ili iwe rahisi kuwafikia matakwa ya serikali ya kuleta maendeleo kwa wananchi. Pamoja na mengine aliyoyazungimza pia amelisisitiza vijana kuacha kutumia fedha hovyo badala yake wakuwekee akiba kupitia VICOBA.

Nao Wawakilishi na viongozi wa Vikundi hivyo wameoneasha kufurahishwa na huduma hiyo ya mikopo waliopokea leo.  Huku wakiomba kampuni hiyo iwape mikopo zaidi kwa ajili ya kufikia malengo yao.

No comments:

Post a Comment