Saturday, May 27, 2017

ENTERTAINMENT: Diamond atoa ushauri huu kwa vijana East Africa , Asema "Naiogopa Kesho"

Diamond akifurahia jambo na mashabiki

Msanii Maarufu Mkali wa 'Marry you' Diamond Platnumz amewaambia vijana wa east Africa kuwekeza zaidi kwenye ubunifu kuliko kufikiri kupata ajira hata kwamba ilhali wamesoma kama hawana ubunifu ni kazi bure.

"Lazima uwe na Kiti cha tofauti na mwingine ili uweze kupata unachodream" , Unapopata jifunze kuwekeza kwa ajili ya kesho" Diamond Platnumz

Alipoulizwa Endapo umaarufu utaisha atajionaje?
"Naiogopa sana , kila nachopata na save kwa ajili ya kesho , nitasaidia kila mmoja maana haujui nani atakusaidia kesho" Diamond Platnumz.
Mashabiki wa Diamond Platnumz
Diamond Amesema hayo mbele ya Maelfu ya mashabiki wake wanafunzi wa chuo cha Nairobi     alipowasili Jana akijiandaa na tamasha la Karoga Festival inayofanyika leo na kumalizika kesho. Diamond atahudhuria Tamasha la pili la Karoga Festival hapo kesho.

Ulikuwa ni mdahalo ulioabdaliwa na kurushwa LIVE na Kituo cha Television ya NTV kwa muda wa zaidi ya dakika 45.

No comments:

Post a Comment