Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeanza kuendesha mchakato wa uteuzi kuwania ubunge wa Afrika mashariki.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo wanawake ndiyo watakao chukua fomu kuwania nafasi Hugo muhimu. Ambapo Mara wanapochukua fomu na kuzirejesha chama kitafanya uteuzi wa kuwania ubunge wa bunge LA Afrika Mashariki (AELA)
Kwa mujibu wa taarifa hiyo Wanachama ambao wana sifa stahiki watatakiwa kuchukua fomu katika ofisi za chama hicho..
"Wanachama hao wenye sifa na vigezo vya kuwania uteuzi nafasi hiyo kupitia CHADEMA watatakiwa kuchukua na kujaza fomu zinazopatikana Ofisi ya Makao Makuu ya Chama Dar es Salaam, Ofisi ndogo za Makao Makuu ya Chama (Zanzibar) ofisi zote za kanda 10 za chama, Tanzania Bara na Zanzibar, Ofisi za Mikoa na Majimbo, kuanzia leo Jumamosi Aprili 29 ambapo mwisho wa kuchukua na kurejesha fomu itakuwa ni Mei 1, mwaka huu, saa 11 jioni." Ilisema taarifa hiyo..
Huku ikieleza mambo ya muhimu anayopaswa kuambatanisha na fomu wakati wakuirudisha Kama inavyoonekana hapo chini.
"1. Fomu iliyojazwa kikamilifu
2. Wasifu wake kamili (CV)
3. Nakala ya ukurasa wa
mwisho wa hati ya
kusafiria/ cheti za kuzaliwa
4. Stakabadhi ya malipo ya
ada ya fomu
5. Nakala ya kadi ya
uanachama
Muombaji anatakiwa kukidhi vigezo na masharti, ikiwa ni pamoja;
a. Awe mwanamke
b. Awe raia wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania
c. Anazo sifa za kustahili
kuchaguliwa kuwa Mbunge
wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania
kwa mujibu wa masharti ya
ibara ya 67 ya Katiba ya
Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania ya mwaka 1977.
e. Asiwe Mbunge wa Bunge la
Tanzania au waziri katika
Serikali wala Mtumishi wa
Jumuiya ya Afrika Mashariki
(EAC).
d. Awe na uzoefu
uliothibitishwa au moyo wa
kupenda kuimarisha na
kuendeleza malengo ya
Jumuiya ya Afrika Mashariki.
e. Akidhi vigezo na masharti
kwa mujibu wa Katiba,
Kanuni na miongozo ya
Chama.
f. Akidhi sharti linalowekwa
na Kanuni za Kudumu za
Bunge Toleo la Januari,
2016; fasili ya 5(3) kuwa
mgombea awe na
uthibitisho
wa uraia wake kutoka Idara
ya Uhamiaji.
Waombaji watakaorejesha fomu na kufanikiwa kuteuliwa watatakiwa kufika au kuwepo jijini Dar es Salaam siku ya Mei 2, mwaka huu kwa ajili ya hatua zingine ikiwa ni pamoja na michakato ya Uhamiaji na Tume ya Taifa ya Uchaguzi."
No comments:
Post a Comment