"Hii ni heshima kubwa sana ambayo ndugu zangu wamenifanyia, kwa kuniweka nipeperushe bendera ya NASA. Tumekuwa na vikao ambavyo vimechukua siku nyingi. Kila kitu tumeandika, tumekubaliana ya kwanza serikali tutakayoiunda, ambayo ni serikali ya mseto itakuwa ni serikali ya mpito,"
"Sisi tuko kama timu, yenye pembe tano (pentagon), wamenipa utepe wa nahodha, hiyo inaniunganisha mimi nao na Wakenya wote, tutatembea pamoja bega kwa bega. Tunataka kubadilisha Kenya na kutekeleza ndoto ya waanzilishi wa taifa letu".
"Tumegundua kwamba muhimu zaidi katika demokrasia ni kuitekeleza. Nilisema awali kwamba niko tayari kuwa hata mtu wa kufagia katika serikali ya NASA, mradu tu raia wa Kenya apate heshima yake. Wananchi wameamua huu ni mwaka wa mabadiliko. Mabadiliko hayo yanaanza nanyi (raia)." Quotes za Raila Odinga.
Raila Odinga |

No comments:
Post a Comment