Friday, April 28, 2017

KIMATAIFA : waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe Kuijadili Korea Kaskazini na Rais Viadmir Putin wa Urusi


Waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe

Waziri Mkuu Shinzo Abe wa Japani amesema yeye na Rais Vladimir Putin wa Urusi wamekubaliana kutoa wito wa pamoja wa kuitaka Korea Kaskazini kujizuia na vitendo zaidi vya kichokozi.


Viongozi hao wawili walizungumza hayo jijini Moscow jana Alhamisi kwenye mkutano wao wa pamoja na waandishi wa habari baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika mapema jana. 

Waziri Mkuu Abe amesema Urusi ni mwanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na mwanachama muhimu wa mazungumzo ya pande sita juu mpango wa nyuklia wa Korea Kaskazini. Mpangokazi huo unaihusisha Japani, Urusi, Marekani, China, Korea Kusini na Korea Kaskazini.

Abe alisema yeye pamoja na Rais Putin wamekubaliana kuendeleza ushirikiano wa karibu kwenye suala la kuitaka Korea Kaskazini kuyaheshimu kikamilifu maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na kujizuia na vitendo zaidi vya kichokozi. 

Viongozi hao pia walijadiliana kuhusu shughuli za kiuchumi za pamoja kwenye visiwa vinavyoshikiliwa na Urusi ambavyo Japani inadai kuvimiliki. 

Waziri Mkuu huyo wa Japani alisema wamekubaliana kutuma kikundi cha maafisa kutoka sekta binafsi na umma kitakachofanya utafiti kwenye visiwa hivyo mapema kuanzia mwezi Mei. Alisema Japani na Urusi zitaanza mchakato wa kufanya miradi ya pamoja iwe thabiti. 

Abe alitoa mfano wa shughuli za ukuzaji wa samaki, samaki wa msumbi na utumiaji wa mazingira tajiri ya asili kwa ajili ya utalii kama mifano ya miradi hiyo. Alisema miradi hiyo itaboresha hali ya maisha na urahisi kwa Warusi wanaoishi kwenye visiwa hivyo. 

Waziri Mkuu huyo alimalizia kwa kusema anatumaini miradi hiyo itatengeneza fursa nyingi kwa Wajapani wanaotumaini kufanya biashara kwenye visiwa hivyo.

No comments:

Post a Comment