Rais Paul Kagame wa Rwanda |
Rais Paul Kagame wa Rwanda amesema urafiki kati ya nchi yake na China ni wa muda mrefu, na serikali na wananchi wake wanashukuru China kwa kuchangia maendeleo ya taifa hilo.
Rais Kagame ameyasema hayo wakati akipokea hati ya utambulisho kutoka kwa balozi mpya wa China nchini humo Bw. Rao Hongwei. Amesema Rwanda inapenda kufanya ushirikiano kati yake na China uingie kwenye ngazi mpya.
Kwa upande wake, balozi Rao amesema katika miaka ya hivi karibuni, uaminifu wa kisiasa kati ya nchi hizo umeongezeka, ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara umeendelezwa kwa kasi na mawasiliano kati ya binadamu yamezidishwa. Ameongeza kuwa katika muda wake wa kazi nchini humo, atatumia fursa zinazotokana na mkutano wa viongozi wa nchi hizo na kutoa mchango mpya kwa ajili ya kupanua na kuimarisha urafiki wa jadi na ushirikiano kati ya China na Rwanda.
No comments:
Post a Comment