Friday, April 21, 2017

Habari: Rais Trump anaamini Xi Jiping atalimaliza suala la Korea Kaskazini

Trump aamini Xi ataweka jitihada kwenye suala la Korea Kaskazini

Rais Donald Trump wa Marekani amesema ana imani kuwa Rais Xi Jinping wa China ataongeza juhudi zake kuishinikiza Korea Kaskazini juu ya mipango yake ya nyuklia na makombora.

Trump alitoa kauli hiyo kwenye mkutano wa pamoja na waandishi wa habari akiwa na Waziri Mkuu wa Italia Paolo Gentiloni jijini Washington, Marekani jana Alhamisi. 

Trump alisema anampenda sana na kumheshimu rais wa China. Alisema wabobezi wote wanasema hawajawahi kuona China ikifanya inachofanya wakati huu kwenye kulishughulikia suala la Korea Kaskazini.

Trump pia alirejelea ukosoaji wake wa mpango wa nyuklia wa Iran ambao ulisainiwa wakati wa utawala wa Obama. Akasema kuwa ni makubaliano mabaya na hayakutakiwa yasainiwe. 

Wakati wa kampeni zake za urais Trump aliashiria kuwa atayafuta makubaliano hayo. Rais huyo amesema Irani haijatimiza kile kilichotarajiwa kwenye makubaliano hayo. Rais huyo amesema utawala wake utaupitia upya mpango huo kuangalia kama una maslahi kwa Marekani.

No comments:

Post a Comment